Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Real shoo sho

Dar es Salaam. Yanga imeona takwimu zisizotisha za Real Bamako inapokuwa katika uwanja wa nyumbani wa Machi 26 jijini Bamako na zikaipa matumaini ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika leo kuanzia saa 1:00 usiku.

Real Bamako katika mechi 16 zilizopita za mashindano ya klabu Afrika ilizocheza nyumbani imeshinda tano, sare nane na kupoteza tatu huku ikifunga mara 18 na kufungwa mabao 12 jambo linaloipa Yanga ari ya kujiamini kama alivyokiri kocha Nasreddine Nabi.

“Tuna kikosi kizuri ambacho kina wachezaji wenye uzoefu na hawahofii kucheza katika uwanja wowote ule na tumeshathibitisha hilo mara kadhaa,” alisema Nabi.

Ushindi utaifanya Yanga kufikisha pointi sita na inaweza kuongoza kundi D au kubakia ya pili jambo litakaloifanya iwe katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali na kuweka rekodi mpya ya kuvuna kwa mara ya kwanza pointi sita katika makundi ya mashindano ya klabu Afrika.

Katika awamu tatu zilizopita ambazo Yanga ilishiriki makundi ya mashindano ya klabu Afrika pointi nyingi ilizokusanya ni nne, hivyo hata ikitoka sare itaifikia rekodi yake ya nyuma.

Vilevile itaweka rekodi ya kushinda mechi mbili za makundi kwani awali iliwahi kushinda mara moja.

Mwamuzi Joshua Bondo (44) ndiye amepangwa kuchezesha mechi hiyo akisaidiwa na Mogomotsi Morakile, Kitso Sibanda na Tshepo Gobagoba, wote wakiwa wanatoka Botswana.

Uwezo wa kufumania nyavu ambao timu hizo zimeonyesha katika mechi za karibuni za mashindano tofauti unatoa ishara kuwa mechi hiyo

huenda isitoke kapa na watazamaji wana nafasi kubwa ya kushuhudia bao au mabao.

Katika mechi tano zilizopita Real Bamako imefunga mabao sita ikiwa ni wastani wa bao moja kila mchezo wakati Yanga imefunga mara saba ikiwa ni wastani wa bao moja kwa mechi.

Safu ya ulinzi ya Yanga inapaswa kuwa makini zaidi katika dakika 15 za mwishoni za kipindi cha kwanza na zile za mwanzoni mwa kipindi cha pili kwani muda huo ndio Real Bamako imekuwa mwiba katika kufumania nyavu.

Katika mabao sita ambazo Real Bamako imepata kwenye mechi tano zilizopita za mashindano ya klabu Afrika - matano imefunga kati ya dakika ya 31 hadi ya 60. Muda ambao Yanga imekuwa hatari zaidi kufunga mabao ndio ambao Real Bamako imekuwa dhaifu zaidi kujilinda jambo ambalo Yanga ikilifanyia kazi zaidi inaweza kupata ushindi.

Katika mabao manne ambayo Yanga imefunga kwenye mechi tano zilizopita za klabu Afrika, mawili imeyapata dakika 15 za mwisho, muda ambao Real Bamako safu yake ya ulinzi imeruhusu mabao matatu kati ya saba iliyofungwa msimu huu.