Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaitumia CR Belouizdad salamu

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI (katikati) akimtoka Issa Ndala wa KMC katika mchezo wa LigiKuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Muktasari:

  • Yanga imejiweka katika hali nzuri kisaikolojia kabla ya kuivaa CR Belouizdad, Jumamosi katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya leo kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya KMC ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Morogoro. Yanga imejiweka katika hali nzuri kisaikolojia kabla ya kuivaa CR Belouizdad, Jumamosi katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya leo kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya KMC ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Hata hivyo, kufuatia ushindi huo namba za alama ilizokusanya Yanga hadi sasa ambazo ni 43 ni kama zimeanza kutishia wapinzani wake kwani inaizidi Simba inayoshika nafasi ya pili kwa pointi saba iliyo na alama 36, ambazo ni sawa na michezo mitatu ili iweze kuwafikia mabingwa hao watetezi wa ligi.

Si hivyo tu, lakini kwa pointi hizo, Yanga inaizidi Azam FC kwa pointi nane sawa na idadi ya michezo mitatu inayopaswa kushinda ili kuifikia.

Yanga iliyoanza mechi hiyo kwa kasi kubwa ilipata bao lake la kwanza katika dakika ya kwanza tu ya mchezo kupitia kwa Mudathir yahya ambaye alimalizia piga nikupige iliyotokea langoni mwa KMC baada ya kipa Wilbol Maseke kufanya kosa la kuondosha vibaya mpira ulionaswa na Pacome Zouzoua na kufanya shambulizi ambalo liliipa Yanga bao hilo la kuongoza.

Katika tukio lililoshangaza wengi, dakika ya 42 kipa wa KMC, Maseke alifanya tukio la lililoshtua wengi la kumtupia ngumi kiungo wake Ibrahim Elias huku naye akijibu mapigo kabla ya wenzao kuwaamulia.

Tukio hilo lilitokea wakati kipa huyo aliyeonekana kutokuwa sawa akiwa na makosa mengi kufanya kosa lingine ambapo Elias alipokwenda kuongea naye akajikuta anaambulia konde hilo.

Mwamuzi wa mchezo huo Omari Mdoe kutoka Tanga naye alitoa kali kwa kushindwa kutoa kadi yoyote kwa wawili hao ingawa baadaye kabla ya kuanza kwa kipindi cha pili KMC ilimtoa kipa huyo na kuingia Denis Richard.

Bao hilo la Yanga lilidumu hadi pale mwamuzi Mdoe alipopuliza filimbi ya kuashiria muda wa mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kupata bao la pili kupitia kwa Mudathir tena safari hii akimalizia pasi safi ya Nickson Kibabage ambaye dakika 6 baadaye beki huyo akatengeneza bao lingine kwa Pacome Zouzoua.

Mashabiki wa Yanga bado wataendelea kusubiri kuona bao la kwanza la mshambuliaji wao mpya Joseph Guede ambaye jana licha ya kuingia katika dakika ya 45 ya kipindi cha pili akichukua nafasi ya Mzize bado aliendelea kutokuwa na bahati ya kuweka mpira wavuni.

Guede alitengenezewa nafasi mbili za wazi, moja kichwa chake kikigonga mwamba huku nyingine kipa Richard akipangua na kuwa kona.

Yanga Imefikisha mabao 39 baada ya ushindi wa jana lakini KMC imechangia mabao 8 kwa mabingwa hao watetezi baada ya kufungwa mechi zote mbili msimu huu,mchezo wa kwanza ikishinda (5-0) na jana kuwafunga tena (3-0).

Baada ya mchezo huo wa jana wa Ligi Kuu kibarua kinachofuata kwa Yanga ni mechi dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria itakayochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumamosi ijayo saa 10:00 jioni.

Mchezo huo utakuwa ni kama fainali kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, kwani watapaswa kushinda ili kuondokana na hesabu za ‘vidole’ ikizingatiwa kwamba hivi sasa wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi D la Ligi ya Mabingwa Ulaya.