Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yakaribia kileleni ikiichapa Fountain

Muktasari:

  • Yanga itaingia tena uwanjani Jumapili ijayo kuvaana na Coastal Union ukiwa ni mchezo wa mwisho kabla ligi haijasimama kupisha michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga imerejea kwenye Ligi Kuu Bara na kupata ushindi muhimu dhidi ya Fountain Gate.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex, Yanga ikiwa na wachezaji wengi ambao hawaanzi kikosi cha kwanza ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

Bao  la kwanza la Yanga kwenye mchezo huo liliwekwa kimiani na Prince Dube kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 29 ya mchezo baada ya beki wa Fountain kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, huku Pacome Zouazoa ambaye aliingia kipindi cha pili akifunga la pili katika dakika ya 82 baada ya kupata pasi safi toka kwa Duke Abuya.

Ushindi huu umeifanya Yanga kusogea hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13, baada ya kucheza michezo mitano imetoka sare mmoja na kushinda minne.

Kileleni kwenye msimamo ipo JKT Tanzania, ambayo imeshacheza michezo 10 na kukusanya pointi 17, huku nafasi ya pili ikishikiliwa  na Pamba ambayo imeshacheza michezo minane na kukusanya pointi 15.

Ushindi huu umeifanya Yanga kuendeleza rekodi yake nzuri ya kushinda mechi 25 mfululizo za Ligi Kuu ambapo imeshinda 23 na kutoka sare mbili tangu ilipofungwa na Tabora United (sasa TRA United), kwa mabao 3-1, Novemba 7, 2024, hii ndiyo timu ambayo imecheza michezo mingi mfululizo bila kupoteza kwa sasa kwenye ligi.

Huu ulikuwa mchezo wa tatu wa ligi wa kocha wa Yanga Pedro Gonçalves, akifanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo yote.

Kipigo hiki kimeifanya Fountain Gate kuendelea kuwa na mwendo wa kusuasua ambapo katika mechi kumi walizocheza hadi sasa, wamepata ushindi mara tatu, kutoka sare moja huku wakipoteza mechi sita na wamefunga mabao manne tu huku wakifungwa mabao 12.

Yanga itaingia tena uwanjani Jumapili ijayo kuvaana na Coastal Union ukiwa ni mchezo wa mwisho kabla ligi haijasimama kupisha michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.