Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yamrudia Aucho kimya kimya

AUCHO Pict

Kiungo mpya wa Singida Black Stars, Khalid Aucho ameshaanza kujifua na timu hiyo mpya iliyompa mkataba wa miaka miwili, lakini kuna jambo linaloendelea kwa mabosi wake wa zamani ambao inadaiwa wanampigia hesabu ya kuendelea kuwa naye.

Aucho aliyeitumikia timu hiyo kwa misimu minne mfululizo aliondoka Jangwani kutokana na kumaliza mkataba aliokuwa nao na ilielezwa alikuwa anajiandaa kwenda Ulaya kumfuata swahiba wake, Kennmedy Musonda anayekipiga kwa sasa Israel kabla ya kuibukia Singida Black Stars.

Hata hivyo, wakati akiwa ameshaanza kujifua na wenzake chini ya kocha wa zamani wa Yanga, Miguel Gamondi, kuna taarifa zimelifikia Mwanaspoti kwamba mabosi wa Jangwani bado wanampigia hesabu kiungo huyo raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 32.

Inadaiwa kuwa ndani ya Yanga baadhi ya mabosi wa timu hiyo, bado wana wasiwasi kama viungo wapya waliosajiliwa hivi karibuni kweli wataweza kuziba ubora wa Aucho ambaye alikuwa injini ndani ya kikosi chao.

Wasiwasi huo umewapa akili kubwa mabosi wa juu wa Yanga ambao wameipa akili Singida Black Stars kumchukua kiungo huyo ili awe kama amekaa njiapanda hivi wakati wakiwasoma viungo wapya.

Yanga baada ya kushindwa kumuongezea mkataba Aucho ilimsajili Moussa Balla Conte, Abdulnassir Mohammed ‘Casemiro’ ambao wanacheza nafasi hiyo ya Aucho.

Hata hivyo, ndani ya Yanga wapo mabosi wanaamini kuwa Conte akipewa muda anaweza kufanya makubwa, lakini lipo kundi lingine bado lina wasiwasi kwamba viungo hao wanaweza kushindwa kuziba pengo la Mganda huyo.

Akili ya Yanga ni kwamba endapo itaonekana Aucho bado pengo lake ni kubwa ni rahisi kumvuta akitokea Singida kuliko angesajiliwa mbali zaidi.

Ili kumweka sawa zaidi Aucho, Yanga ilishamalizana naye vizuri kwa wema ikimpa hadi tuzo ya kutambua ubora wake huku kiungo huyo akimaliza zaidi aliposema hatahamia timu hasimu na mabingwa hao.

“Tunataka kuendelea kuwaangalia hawa viungo wapya. Unajua kuziba pengo la Aucho kwa haraka ni kitu tunachokiombea kifanikiwe,” alisema bosi huyo wa juu wa Yanga na kuongeza:

“Unajua uamuzi wa kutomuongezea mkataba Aucho ulitokana na namna alivyocheza msimu uliomalizika. Kuna wakati tulimkosa ilituumiza kutokana na majeraha. Hakuna shida kati ya Yanga na Aucho ndio maana mliona hata rais wetu (Hersi Said) alimpa tuzo na hakuna ugumu kwetu kumpata mchezaji kutoka Singida tuna uhusiano nao mzuri.”

Aucho alijiunga na Yanga Septemba 2021 akitokea Masr El Makasa ya Misri na kutwaa mataji zaidi ya 10 Jangwani yakiwamo manne ya Ligi Kuu Bara na mengine kama hayo ya Kombe la Shirikisho Bara (FA), mbali na Ngao za Jamii tatu, Kombe la Mapinduzi, Kombe la Muungano na Kombe la Toyota walilotwaa msimu uliopita nchini Afrika Kusini.