Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yavunja rekodi ya Pamba Jiji ikiipiga tatu

Kiungo wa Yanga, Duke Abuya wakati akitoa pasi katika mechi ya Ligi Kuu ambayo Yanga imeshinda 3-0 dhidi ya Pamba Jiji. Picha na Yanga

Muktasari:

  • Yanga imeendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikifikisha pointi 44 ambazo imekusanya katika mechi 18, ikishinda mechi 13 na kutoka sare tano.

Rekodi ya Pamba Jiji FC kutopoteza mechi nyumbani katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu imefikia tamati leo Jumatano, Aprili 8, 2026 baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kabla ya kichapo cha leo, Pamba Jiji ilikuwa haijapoteza mechi tisa za Ligi uwanjani hapo ikipata ushindi katika mechi tano na kutoka sare nne.

Walioitoa kimasomaso Yanga katika mechi ya leo ni viungo Mudathir Yahya ambaye amepachika mabao mawili na Maxi Nzengeli ambao wote wamefunga wakimalizia pasi za kiungo Allan Okello.

Bao la kwanza limefungwa katika dakika ya nane na la pili katika dakika ya 33 yote yakiwa ya Mudathir na la tatu limefungwa na Nzengeli katika dakika ya 67.

Matokeo hayo ya leo yameifanya Yanga sasa ihitaji pointi tano tu katika mechi 12 ilizobakiza ili ijihakikishie rasmi kutoshuka daraja pasipo kutegemea matokeo ya timu nyingine.

Pia Yanga imeendeleza rekodi yake ya kibabe ya kutopoteza mechi kwenye Ligi Kuu ikifikisha mechi ya 38.

Mkoani Singida katika Uwanja wa Airtel, wenyeji Singida Black Stars wametoka kifua mbele kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC.

Bao pekee la ushindi la Singida Black Stars katika mchezo huo limepachikwa katika dakika ya 70 na Lamin Jarjou akimalizia mpira uliiokolewa na beki wa KMC, Nickson Mosha baada ya shuti la Ayoub Lyanga.

Ushindi huo umeifanya Singida Black Stars kufikisha pointi 28 na kusogea hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wakati huo KMC ikizidi kubakia mkiani mwa msimamo wa ligi na pointi zake nane.