Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega akiwa na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda wakijadiliana kabla ya kuanza kwa kikao cha bodi ya barabara ya mkoa huo kinachofanyika jijini Arusha leo Jumatatu, Januari 6, 2025.
Waziri Ulega yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kukagua barabara, akiambatana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Aisha Amour na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mohamed Besta.