Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya leo Jumanne, Julai 7, 2026 amewatembelea na kuzungumza na maofisa usafarishaji maarufu Bodaboda wilayani humo ambao, wameonekana wakiendelea na shughuli za usafirishaji kama kawaida.
Bulaya amewatembelea bodaboda hao huku akiwataka kuhakikisha amani inadumishwa ili kuchochea uchumi huku akisisitiza tofauti za vyama na za kiitikadi hazipaswi kupewa nafasi kuvuruga amani.