Hali ya utulivu imeshuhudiwa katika maeneo ya ubungo katika daraja la Kijazi , jijini Dar es Salaam, leo Julai 7, 2026, majira ya saa 2:00 asubuhi, magari na watembea kwa miguu wakionekana kwa uchache kuliko ilivyo kawaida.
Photo: 1/10
Wananchi wakiendelea na shughuli zao katika Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam.
Photo: 2/10
Licha ya hali kuonekana kuwa shwari katika maeneo ya Chanika na viunga vyake, daladala nyingi zinazofanya safari ya kwenda mjini zimeonekana kuegeshwa katika eneo la sheli Chanika Mwisho.
Photo: 3/10
Daladala zikishusha na kupakia abiria katika kituo cha Tabata Mwananchi.
Photo: 4/10
Leo Julai 7, 2026 eneo la Tabata Kisiwani, Dar es Salaam majira ya 4:00 asubuhi linaonekana kuwa na utulivu huku baadhi ya wakazi wakiendelea na shughuli zao za kila siku.
Photo: 5/10
Photo: 6/10
Barabara ya Mwenge-Tegeta eneo la Tangi Bovu.
Photo: 7/10
Photo: 8/10
Polisi wakiwa na pikipiki katika doria eneo la Chanika.