Kwa mara nyingine mwigizaji na mwandaaji wa filamu nchini, Idris Sultan ameingia tena kwenye soko la filamu la kimataifa baada ya filamu aliyoshiriki ya Married To Work kuingia kwenye jukwaa kubwa la usambazaji na uonyeshaji wa filamu duniani, la Netflix.