Matukio mbalimbali wakati wa kuhesabu kura na kutangazwa Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma leo.
Wahudumu wa Bunge wakiwa wamebeba masanduku ya kura za wabunge walizopiga kumchaguwa Waziri Mkuu mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa wakizipeleka kuhesabiwa, mjini Dodoma leo asubuhi. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 1/13
Waziri Mkuu mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) akiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju wakitoka katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 2/13
Watumishi wa Bunge wakifanya kazi za kuhesabu kura zilizopigwa na wabunge kuidhinisha jina la Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano,mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 3/13
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akielekea kula kiapo cha utii baada ya kupitishwa na bunge kushika wadhifa huo, mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 4/13
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akila kiapo cha utii mbele ya Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kupitishwa na bunge kushika wadhifa huo, mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 5/13
Waziri Mkuu mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa akiwashukuru wabunge kwa kumuidhinisha kushika wadhifa huo, bungeni mjini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 6/13
Wabunge wakiwa wamesimama wakiangaza macho huku na huku kuangalia alipoketi Waziri Mkuu aliyependekezwa na Rais ambaye ni Majaliwa Kassim Majaliwa. Majaliwa hakuwepo bungeni wakati jina lake likisomwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 7/13
Spika wa Bunge, Job Ndugai akisoma jina la Waziri Mkuu aliyependekezwa na Rais ambaye ni Majaliwa Kassim Majaliwa. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 8/13
Spika wa Bunge, Job Ndugai akionyesha barua ya Rais John Magufuli aliyoiandika kwa mkono wake kabla ya kuanza kuisoma. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 9/13
Spika wa Bunge akionyesha baasha aliyoipokea kutoka kwa mpambe wa Rais John Magufuli iliyokuwa na jina la Waziri Mkuu aliyempendekeza Majaliwa Kassim Majaliwa. Barua iliyokuwa na jina la Maliwa ilikuwa imefungwa kwenye baasha tatu. Picha na Edwin mjwahuzi
Photo: 10/13
Askari wa Bunge wakimuongoza mpambe wa Rais John Magufuli kuingia bungeni na barua ya rais iliyokuwa na jina la Majaliwa Kassim Majaliwa aliyempendekeza kuwa Waziri Mkuu . Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 11/13
Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozwa na askari wa bunge kuingia ukumbini kuongoza kikao cha tatu cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 11, mjini Dodoma tayari kwa kuwasiliswa bungeni kwa jina la Waziri Mkuu. Picha na Edwin Mjwahuzi
Photo: 12/13
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah (kushoto) na Naibu Katibu wa Bunge, John Joel wakirejea bungeni baada ya kumaliza kuweka utaratibu jinsi barua ya Rais John Magufuli itakavyoingizwa bungeni iliyoiandika kwa kupendekeza jina la Waziri Mkuu. Picha na Edwin Mjwahuzi