Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (wa pili kulia) akisalimia wananchi wakati maandamano ya wafuasi wa chama hicho yalipokuwa yakipita Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, leo. Chadema wameandamana kupinga miswada ya sheria za uchaguzi iliyowasilishwa bungeni.