Wanafunzi wa Shule ya Msingi Amani iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani wakisikiliza viongozi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Abubakari Kunenge walipotembelea shule hiyo kujionea hali baada ya kufunguliwa rasmi kwa shule za msingi na sekondari nchini. Uandikishaji wa wanafunzi wanaoanza elimu ya awali na msingi kwenye shule za Serikali Mkoa wa Pwani unatarajia kuendelea hadi ifikapo mwezi machi mwaka huu. Picha na Sanjito Msafiri