Simanzi imetawala wakati wa kuomboleza na kumuaga Rais wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi ambapo viongozi na wananchi wamejitokeza kumuombea na kumuaga katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam leo Machi 1, 2024. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amewaongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo aliyefariki jana Februari 29, 2024.