Msongamano uliosababisha abiria kuchelewa umesababisha matumizi ya tiketi za kawaida kurejea katika Stendi ya mabasi ya Magufuli, mfumo huo ulianza Jumatatu ya Februari 20, 2023 lakini umekuwa ukilalamikiwa kutokana na kuwekwa kwenye geti moja tu jambo linalosababisha msongamano.