Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amewakaribisha rasmi wanafunzi wa shule mpya ya Sekondari ya Wasichana Manyara kwa kuvaa sare za shule hiyo ili kuwapa hamasa ya kusoma. Sendiga amewakaribisha rasmi wanafunzi hao 110 wa kidato cha tano mjini Babati leo Agosti 14 mwaka 2024 waliokwishawasili shuleni hapo na kuanza masomo yao ya kidato cha tano kwa mchepuo wa Sayansi (PCM) na (PCB). Picha na Joseph Lyimo