Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, leo Ijumaa Julai 17, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, katika makazi yake yaliyopo Mbezi Juu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari cha Ofisi ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu wa Zanzibar, alifika nyumbani kwa Jaji Warioba kwa lengo la kumjulia hali na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu nchi.