BIASHARA: Wanawake wakipepeta pumba za mpunga eneo la Mabatini jijini Mwanza ili kupata chenga za mchele zinazotumika kupikia uji na vitumbua. Kilo moja ya chenga hizo huuzwa kati ya Sh600 hadi Sh1,000. Picha na Michael Jamson.
Photo: 1/7
KIAPO: Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu Harlod Nsekela (kushoto) akiwaongoza makamishna wapya wa Idara ya Uhamiaji kula kiapo cha maadili ya viongozi wa umma baada ya kuapishwa mjini Dodoma jana. Picha na Ben Patrick
Photo: 2/7
CHANGAMOTO: Wachuuzi wa vifaa mbalimbali ikiwamo vya magari wakiwa wamening’inia nyuma ya lori la mafuta lililokuwa kwenye foleni katika Barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam, kitendo hicho kinaweza kuhatarisha maisha yao. Picha na Said Khamis
Photo: 3/7
TWENDE HUKU WEWEEE...Polisi wakimkamata Selemani Said Nassoro katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi baada ya kuachiwa huru katika kesi ya mtandao iliyokuwa inamkabili. Alikamatwa tena ili afunguliwe kesi nyingine. Picha na Omar Fungo
Photo: 4/7
Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ (katikati) akiwa na ndugu, jamaa na marafiki zake wakati akitoka Kituo Kikuu cha Polisi baada ya kuachiwa huru, jana jijini Dar es Salaam. Picha na Salim Shao
Photo: 5/7
UGAIDI: Watuhumiwa wa kesi za matukio ya ugaidi ikiwemo urushwaji wa mabomu katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha wakipanda gari kwa ajili ya kurejeshwa gerezani baada ya kesi yao kuhairishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, jana. Picha na Zulfa Musa
Photo: 6/7
BIASHARA YA SAMAKI: Mchuuzi wa samaki katika Soko la Feri, jijini Dar es Salaam akiwa amebeba samaki aina ya chuchunge kabla ya kumuuza sokoni hapo juzi. Picha na Salim Shao