Juni 16 ya kila mwaka ni siku ya Mtoto wa Afrika. Na leo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameadhimisha siku hiyo pamoja na wajukuu zake katika Ikulu ya Dar es Salaam na kushiriki nao michezo mbalimbali. Rais Samia amekuwa kama mwalimu kwa kuwapa kazi mbalimbali za kufanya kisha kuwatembeza Ikulu hiyo kujionea ilivyo ikiwemo ofisini kwake.