Rais Donald Trump amezindua rasmi ndege mpya ya Rais wa Marekani, Air Force One, ambayo awali ilikuwa mali ya familia ya kifalme ya Qatar, kabla ya kutolewa kama zawadi kwa Serikali ya Marekani.
Ndege hiyo aina ya Boeing 747-8 imeelezwa kuwa moja ya ndege za kifahari zaidi kuwahi kutengenezwa duniani, ikiwa na thamani inayokadiriwa kufikia dola 400 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1 trilioni).