Miongoni mwa Wajumbe sita wa Jumuiya ya Wabunge wa Bunge la Canada wanaoshughulikia masuala ya Afrika, Taleeb Noormohamed na Brenda Shanahan wakifurahi jambo wakiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtopepo iliyopo Zanzibar wakati ujumbe huo ulipotembelea shule hiyo, Februari 22, 2024. Katika ziara hiyo ya Wabunge hao walijionea walimu waliopata mafunzo ya stadi za maisha wakitoa elimu ya stadi za maisha kuhusu afya ya uzazi na jinsia na kujilinda na vitendo vya ukatili kwa wanafunzi wa shule za msingi na wanafunzi walionyesha uelewa wao na matumizi ya stadi za maisha. Picha na UNICEF