Mkazi wa Kata ya Mwembesongo kutoka jamii ya wafugaji, Habakuki Lemanya akiwa amewashika mkono watoto wake, Grace (kulia) anayeanza darasa la kwanza na Zelisha anayesoma darasa la nne wakati akiwapeleka Shule ya Msingi Mwembesongo iliyopo mkoani Morogoro. Shule za msingi na Sekondari zimefunguliwa rasmi leo Januari 8, kwa ajili ya muhula mpya wa masomo wa mwaka 2024. Picha na Juma Mtanda