Azam Pesa kuleta mapinduzi katika ujumuishaji, uhuru wa kifedha

Ukuaji wa sekta ya fedha katika miaka kadhaa iliyopita kumesaidia ukuaji wa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja kwa maana ya idadi ya wanufaika wa mnyororo wa thamani wa sekta hiyo.

Mbali na ukuaji huo lakini changamoto bado ipo katika ujumuishaji wa huduma za kifedha ambapo kundi kubwa la wananchi hususani wanaoshi vijijini limeonekana kutengwa na ukuaji huu kutokana na sababu mbalimbali.

Sababu hizo zinatajwa kuwa ni ufikaji mdogo wa huduma za kifedha, elimu kuhusiana na huduma za kifedha pamoja na miundombinu ya ufikishaji wa huduma hizo katika maeneo hayo.

Kutokana na changamoto hizo, AzamPesa inafanya juhudi kubwa ya kuhakikisha ujumuishaji wa kifedha unakuwa ajenda kuu ili wananchi wengi waweze kufikiwa na huduma hizo.

Meneja Mauzo wa Azam Pay Kitengo cha Malipo, Shadrack Kamenya anasema AzamPesa ni huduma ya fedha kwa njia ya simu inayopatikana kwenye iOS na Google Play.

“AzamPesa inampa mteja njia rahisi na ya uhakika ya kutuma/kutoa pesa, kulipa bili, kununua muda wa maongezi, kupata huduma za kibenki, kufanya malipo ya Serikali na kulipia huduma za Azam,” anasema Kamenya.

Anasema mteja anaweza kujisaijili na AzamPesa kirahisi kwa kufuata hatua chache, ikiwa ni pamoja na usajili binafsi kwa kufika kwa wakala wa AzamPesa ukiwa na namba ya kitambulisho cha Taifa au kwa kupakua programu tumishi (App) ya AzamPesa inayopatikana kwenye iOS na Google Play.

“Ukiwa na AzamPesa, unaweza kusimamia mahitaji yako yote ya kifedha kutoka sehemu moja cha muhimu ni kuhakikisha una simu ya mkononi pamoja na laini ya mtandao wowote iliyosajiliwa,” anasema Kamenya.

Lengo la AzamPesa ni kupanua wigo wa utoaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu katika eneo kubwa la Tanzania pamoja na kuongeza ujumishaji wa huduma za kifedha.

“Tumejidhatiti kuhakikisha kwamba tunaongeza wigo wa matumizi ya huduma za kifedha kidijitali kwa kutengeneza thamani ambazo zinakidhi mahitaji ya soko la huduma za fedha nchini na kuwahamasisha Watanzania kutumia huduma za kifedha za kidijitali,” anasema Kamenya.

“Ikiwa ni kampuni ya kwanza na pekee ya utoaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu kwa kutumia laini za kampuni yoyote nchini, huduma na bidhaa zetu zimebuniwa kuendana na mahitaji ya wadau wote na gharama nafuu ili kuwawezessha Watanzania wote kushughulikia changamoto zao za kifedha za kila siku,” anasema Kamenya.

Kamenya anasema kupitia AzamPesa mteja anaweza kulipia huduma na bidhaa mbalimbali, kutuma pesa, kununua vifurushi, kulipa bili kwa gharama nafuu zaidi ukilinganisha na mitandao mingine iliyopo sokoni.

AzamPesa ina mawakala nchi nzima wanaowezesha wateja kufanya miamala mbalimbali pamoja na huduma nyingine ikiwemo za wateja wakubwa ambao wanafanya malipo ya pamoja (bulk payments).

AzamPesa ndiyo kampuni pekee nchini ambayo imeweka zawadi mbalimbali za kifedha (incentives) ili kuwahamasisha wafanyabiashara wa maduka ya rejareja kutumia njia za kidijitali katika kufanya miamala.

Kwa AzamPesa uhuru wao ni kumpa mteja njia mbalimbali za malipo kwa urahisi na haraka kupitia “Pochi” ya AzamPesa. Pia mteja anaweza kufanya malipo kupitia njia ya MasterQR Code wakati wowote.