Haki na wajibu wa watumiaji wa usafiri wa anga viko katika mikono salama ya TCAA-CCC

Muktasari:

Watumiaji ni kundi muhimu kati­ka ukuaji na Maendeleo ya biashara yoyote duniani iwe ya huduma ama bidhaa.Hili ni kundi la watu au mtu wanaonunua bidhaa au huduma kwa mahitaji yao.

Watumiaji ni kundi muhimu kati­ka ukuaji na Maendeleo ya biashara yoyote duniani iwe ya huduma ama bidhaa.Hili ni kundi la watu au mtu wanaonunua bidhaa au huduma kwa mahitaji yao.

Mtumiaji hawezi kuuza tena bidhaa au huduma aliyonunua lakini anaweza kuitumia ili kupata riziki yake na kujia­jiri. Mtumiaji ndiye mtu wa mwisho kutumia bidhaa au huduma yoyote.

Katika uchumi wa soko, mtumiaji hununua bidhaa au huduma hasa kwa matumizi na si kwa ajili ya kuuza tena au kwa madhumuni ya kibiashara.

Kwa hivyo, watumiaji wana jukumu muhimu katika mfumo wa kiuchumi na kuunda sehemu ya msingi ya uchu­mi wowote duniani. Bila mahitaji ya watumiaji, wazalishaji wangekosa moja wapo ya motisha muhimu za kuzalisha na kuuza.

Sekta ya usafiri wa anga nchini kama zilivyo sekta nyingine inaongozwa na watumiaji kwa sababu wao ndiyo wanaamua kampuni gani ya kutumia kwa ajili ya safari za ndani na nje ya nchi.

Kwa kutambua umuhimu wa watu­miaji wa huduma za usafiri wa anga, Serikali iliamua kuunda Baraza la Ush­auri la Watumiaji wa Huduma za Usafi­ri wa Anga Tanzania (TCAA-CCC).

Wakati tukiwa katika maadhimisho ya Siku ya Usafiri wa Anga Duniani, gazeti hili lilifanya mahojiano maalu­mu na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Innocent Kyara ambaye pamoja na mambo mengine alieleza majukumu na umuhimu wa baraza hilo kwa watu­miaji wa huduma za usafiri wa anga nchini.

TCAA-CCC lilianzishwa lini na lina majukumu gani?

TCAA-CCC ni chombo cha Serikali kilichoundwa kwa mujibu wa sheria ya Usafiri wa Anga sura ya 80 kama ili­vyofanyiwa marekebisho mwaka 2020 kwa ajili ya kuwakilisha na kutetea maslahi ya watumiaji wa huduma za usafiri wa anga nchini.

Baraza lina jukumu la kuwakilisha maslahi ya watumiaji wa huduma za usafiri wa anga kwa kushauriana na mamlaka husika (TCAA), waziri mwe­nye dhamana ya mambo ya usafiri wa anga katika mambo yanayogusa maslahi ya mtumiaji.

Kupokea na kuwasilisha taarifa na maoni kuhusu masuala ya msingi ya watumiaji wa huduma za usafiri wa anga.

Kuanzisha kamati za watumiaji kati­ka kanda na mikoa na kushauriana na kamati hizo.

Kufanya mashauriano ya kina na wahusika katika sekta ya usafiri wa anga, Serikali pamoja na makundi mengine ya watumiaji wa huduma ya usafiri wa anga kuhusu masuala ya msingi na kero mbalimbali za watu­miaji katika sekta.

Ni changamoto gani ambazo watu­miaji huziwasilisha mara nyingi kwa baraza?

Zipo changamoto nyingi ambazo watumiaji wa huduma za usafiri wa anga hukutana nazo katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini lakini zipo ambazo malalamiko yake hutokea mara kwa mara ambazoni; kuchelewa kwa ndege kwa mujibu wa ratiba na mkataba wa safari, upotevu, uche­leweshwaji na uharibifu wa mizigo ya abiria, kuahirishwa mara kwa mara kwa safari za ndege na mawasiliano duni yaliyopo kati ya watoa huduma na abiria pindi yanapotokea mabadi­liko.

Ili kushughulikia changamoto hizi, baraza huwa linatumia vikao na miku­tano mbalimbali na watoa huduma na kutoa ushauri wa njia bora za kutumia ili kukabiliana na changamoto hizo jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubw akupunguza malalamiko hayo hususani upotevu wa mizigo na mali za abiria.

Pia huwa tunawashuauri abiria kuwa na bima za safari kwa sababu zitawasaidia kulipwa fidia pindi chan­gamoto kama hizi zikitokea.

Ni njia gani ambazo watumiaji wa usafiri wa anga wanazitumia kuwasili­sha changamoto zao kwa baraza?

Kutokana na ukuaji wa teknolo­jia baraza lina mfumo wa kupokea malalamiko ya watumiaji kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa huduma za Serikali kimtandao.

Mfumo tunaotumumia katika kupokea malalamiko ya watumiaji unaitwa E-Mrejesho ambao ni jukwaa maalumu linalosaidia umma kuweza kufikia huduma mbalimbali za Serikali kwa kutumia program tumishi (App) ambayo inapatikana kwenye Playstore au Appstore.

Baada ya kupakua App hiyo mtu anaweza kuifungua na kuangalia ukurasa maalumu wa TCAA-CCC na kuweka malalamiko yake. Pia mtu asiyetumia simu janja (smartphone) anaweza kupata huduma ya kuwasili­sha malalamiko yake kwa kupiga *152*00#.

Pia mtumiaji anaweza kutoa malalamiko yake kwa mtoa huduma kwa njia ya maandishi akiambatani­sha vielelezo muhimu vinavyohusu lalamiko lake na kutuma nakala kwa baraza, kutembelea ofisi za baraza zilizopo Jengo la TBA, barabara ya Ali Hassan Mwinyi Kinondoni, kupiga simu bure 0800110190, kutembelea mitandao ya kijamii ya baraza; Ins­tagramtcaa_ccc,Twittertcaa_ccc1aut­ovutiyawww.tcaa-ccc.go.tz.

Je? Baraza lina ushirikiano na taasisi za ndani na nje katika muktadha wa kubadilishana maarifa

Ndiyo. Baraza lina ushirikiano na taasisi mbalimbali jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio yetu.

Tumekuwa tukishirikiana na wadau wote kwa sababu tuko katika mfumo wa utatu (Serikali, watoa huduma na watumiaji) ambapo kupitia mfumo huu baraza limekuwa likiandaa miku­tano, warsha na vikao mbalimbali vyenye lengo la kushauriana namna ya kushughulikia malalamiko ya watu­miaji.

Aidha, baraza ni mwanachama wa umoja wa jukwaa la mtumiaji Tan­zania (Tanzania Consumer Forum) ambacho ni chombo kinachokutanisha mabaraza na taasisi za Serikali zinaz­olinda watumiaji nchi nzima.

Kupitia umoja huo kumekuwa na vikao na mikutano mbalimbali ya wenyeviti, makatibu na wajumbe wa mabaraza hayo ambayo hufanyika mara nne kwa mwaka kwa lengo la kujadili maslahi na changamoto za watumiaji.

Kwa nje ya nchi baraza limeku wa naushirikiano na taasisi za watumiaji wa usafiri wa anga Afrika Mashariki, Umoja wa Usafiri wa Anga Afrika na vyama vingine.

Ni vitu gani ambavyo Baraza imepan­ga kufanya wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usafiri wa Anga Duniani?

Baraza linatarajia kuangalia kwa vitendo hatua mbalimbali ambazo abiria anatakiwa kupita akiwa uwanja wa ndege. Zoezi hilo litafanyika katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa lengo la kutambua changamoto wanazokutana nazo watumiaji wa usafiri wa anga.

TCAA-CCC ina dhamira ya kuwa­jengea uwezo watumiaji wa huduma za usafiri wa anga nchini kwa kuten­geneza mazingira mazuri ya kushau­riana kuelimishana na uwakilishi ili kuhakikisha haki na wajibu wa mtu­miaji katika soko la usafiri wa anga zinazingatiwa.