Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kusheherekea urithi wa matumaini: Dk Jane Goodall afikisha umri wa miaka 90

Dk Jane akizungumza wakati wa tukio la Roots & Shoots lililofanyika katika hafla ya Taasisi ya Jane Goodall (JGI), Jijini Chicago Machi 23, 2019. Picha kwa hisani ya: JGI Mary Paris

Tunafuraha na heshima kubwa kuwaletea mwanahistoria na mtafiti mashuhuri wa sokwemtu na mwanaharakati wa kuhifadhi mazingira, Dk Jane Goodall.

Kwa zaidi ya miaka 60 iliyopita, Jane Goodall alitembelea kwa mara ya kwanza katika ufukwe wa pale ambapo leo ni Hifadhi ya Taifa ya Gombe nchini Tanzania kuanza utafiti wake wa kihistoria kuhusu tabia za sokwe.

Katika miongo sita iliyopita, utafiti huu umebadilisha mitazamo ya kisayansi kuhusu uhusiano kati ya binadamu na wanyama wengine. Leo, lengo la Dk Jane Goodall limepanuka na kuhamasisha juhudi ya kuwawezesha kila mtu kufanya dunia iwe mahali bora kwa watu, wanyama wengine, na sayari tunayoishi.

Mwana 1977, Dk. Goodall alianzisha Taasisi ya Jane Goodall (JGI), kati ya taasisi kongwe ulimwenguni katika kulinda sokwe na mazingira yao kupitia mbinu ya uhifadhi shirikishi za kuhusisha jamii inayojulikana kama ‘Tacare’.

Taasisi hii inafanya kazi kupitia matawi 24 ulimwenguni kufahamu zaidi kuhusu Wanyama wapatikanao katika Hifadhi ya Gombe. Hifadhi hii imekuwa maarufu kwa utafiti wa muda mrefu zaidi ulimwenguni wa sokwemtu waishio porini.

Hii ni pamoja na kuwawezesha vijana kupitia mpango wa Roots & Shoots wa Jane Goodall uliopo katika nchi 70 ulimwenguni ili kuwajengea uelewa wa kuhifadhi Wanyama, misitu na kuwasaidia wanadamu.

Roots & Shoots inasherehekea imetimiza ya miaka 33 na Tacare inasherehekea kumbukumbu yake ya miaka 30 mwaka huu. Kabla ya janga la UVIKO-19, Dk Goodall alikuwa akisafiri karibu siku 300 kwa mwaka kwenye ziara ya kuongea ya ulimwengu.

Kufuatia vizuizi vya kusafiri vilivyotokana na janga hilo, Jane na taasisi ilianzisha mradi wa ‘Jane Mtandao’ – njia ya kuungana na hadhira kwa njia ya mtandao kutoka nyumbani kwake Bournemouth, Uingereza ambapo alikulia.

Dk Jane amewafikia watu wengi duniani kupitia mihadhara ya kielektroniki, mahojiano na vyombo vya habari na podcast yake maarufu, ‘Jane Goodall Hopecast.’ Jane ni Mjumbe wa Amani wa Umoja wa Mataifa, na Bibi wa Milki ya Falme ya Kiingereza na hivi karibuni amekuwa Mshindi wa Tuzo ya Templeton ya 2021.

Hakika, tuzo na heshima zake ni nyingi sana kuziorodhesha. Akiwa mwandishi hodari wa vitabu, ameandika kitabu kipya kiitwacho, ‘Kitabu cha Matumaini: Mwongozo wa Kuishi Kipindi chenye Changamoto,’ kilichochapishwa, wakati wa majira ya vuli ya mwaka 2021. Tunakualika kuungana nasi kuadhimisha miaka 90 ya kuzaliwa kwa mtu maarufu ulimwenguni, Dk Jane Goodall.


Hazina ilioanzia Tanzania

Akiwa na miaka 26, Dk Jane Goodall alianza safari kutokea Uingereza ambayo ingekuwa msingi wa utafiti wa sokwemtu, akileta mtazamo mpya wa jumuiya ya kisayansi unaofafanua mahali pa binadamu katika ulimwengu wa asili.

Uchunguzi wake wa kihistoria, kwamba sokwemtu hutengeneza na kutumia zana uliondoa vizuizi vya mitazamo vilivyokuwepo kati yetu na jamii za wanyama, badala yake kusisitiza urithi wetu wa pamoja na changamoto zake. Baada ya miaka kupita lengo jipya la Dk.

Dk Jane Goodall akiwa na Sokwe Freud katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe nchini Tanzania. Picha kwa hisani ya: Michael Neugebauer

Jane Goodall limejumuisha wito wa uhifadhi, ushuhuda wa upendo wa dhati kwa Tanzania na hazina zake. Kituo cha Utafiti cha Gombe, mahali ambapo ugunduzi huu ulianzia, kinasimama kama taa ya tumaini na ishara ya uhusiano thabiti kati ya Dk. Jane Goodall na ardhi iliyolinda ugunduzi wake.

Utafiti huu wa mabadiliko unaendelea hadi sasa ukiwa utafiti mrefu zaidi ulimwenguni wa sokwemtu wanaoishi katika mazingira yao ya asili.


Mapenzi yake kwa mbwa:

Ingawa jina la Jane linahusishwa zaidi na sokwemtu, alianza kwa kumpenda mbwa ambaye alijifunza mambo mengi toka kwake.

Anakiri kwamba alipokuwa mdogo, maandalizi bora kuwaelewa wanyama yalitoka kwa mbwa wake, Rusty. Kama vile mbwa anaweza kuwa rafiki bora wa mmiliki wake, hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Rusty. Lakini zaidi ya hayo, wakati Jane akimchukua Rusty kutembea, majukumu yao yalibadilika na kuwa Rusty ndiye alikuwa akimchukua Jane kutembea.

Rusty angeongoza, na Jane angefuata, akimtazama na kujaribu kuelewa ni nini kilimfanya Rusty achague njia hii badala ya ile, ni nini kilikuwa cha kuvutia kwa mbwa, ni tabia za kipekee katika ulimwengu wa Rusty. Na Rusty pia alimfundisha Jane kwamba mbwa wana utu wa kipekee, kuna utofauti kwa kila mmoja.

Na vitu hivi vyote vilikuwa na nguvu kubwa wakati Dk Jane alipokuwa akiishi na sokwemtu, alitambua kwamba sokwemtu wangemfundisha majibu, na kweli wakamfundisha hayo na mengi zaidi. Na hivyo safari ya maisha yake, kutoka kwa mbwa hadi sokwe na misitu hadi mfumo mzima wa bayoanuai na ustawi wa watu, imemuacha na kazi rahisi lakini kubwa – kufanya maisha kuwa bora kwa kila kiumbe hai.

Na hivyo kusifu mwanzo wake, hivi karibuni alikwenda kwenye ufukwe wa bahari huko California na mbwa 90 walioletwa na wamiliki wao kuadhimisha miaka 90 ya Dk Jane, kwa maana halisi, Salamu ya Mbwa 90!


Nadharia ya Matumaini

Kuna sababu kwa nini hadithi ya Dk Jane Goodall inagusa hisia za mioyo mingi sana – imeandikwa kwa dhana ya tumaini lisiloshindwa na shauku isiyoweza kufifia.

Kila mwaka unavyopitia, azimio lake linachochewa zaidi, likiongozwa na utambuzi kwamba wakati ni kifungu ambacho yeye na sisi, hatuwezi tena kumudu kupoteza. Akiikabili miaka yake ya jioni, Dk Jane Goodall anatumia nguvu zake kwa bidi zaidi, akijua kwamba kila wakati ni fursa yenye thamani ya kipekee ya kuhamasisha kwa ajili ya sayari dunia na wakazi wake.

Hisia hii inaonekana pia katika mioyo ya wale waliozishuhudia kazi zake. Kutoka kwa roho zilizokata tamaa ambazo zimepata kusudi jipya katika mihadhara yake, hadi watu bila idadi waliohamasika na neno lake lililoandikwa, Dk Jane Goodall anabadilisha kukata tamaa kuwa hatua, akionyesha matokeo makubwa ya kujitolea kwa mtu mmoja kwa mabadiliko.

Kutoka Tanzania hadi Jukwaa la Kimataifa Mpango wa Roots & Shoots, ulianza katika ardhi ya Tanzania na kikundi cha wanafunzi kumi na wawili, hadi sasa umeenea ulimwenguni kote ambako upo katika zaidi ya nchi 70.

Kazi hii inadhihirisha falsafa ya Dk Jane Goodall: kwamba kila mtu anaweza kuleta mabadiliko tofauti kila siku ya maisha yake, na kwamba ni juu ya mtu binafsi kuchagua tofauti anayotaka kufanya, akiwa na uwezo wa kuleta mabadiliko.

Ni harakati ambayo ilianza ndani ya Afrika lakini sasa inaendelea ulimwengu kote, ikihamasisha hatua kuelekea mustakabali wa mazingira endelevu. Vivyo hivyo, mipango ya uhifadhi inayoongozwa na jamii ya Taasisi ya Jane Goodall, iliyozinduliwa na Dk Jane Goodall na timu yake nchini Tanzania, inaonesha ufanisi wa kina wa kuhusisha jamii za ndani katika uhifadhi na ulinzi wa mazingira yao.

Mbinu ya Tacare ni mfano wa uhifadhi unaoheshimu muunganiko wa ustawi wa binadamu na asili, umeweka kielelezo cha ulimwengu kwa maendelo endelevu na uhifadhi wa mazingira.


Fahari ya Tanzania, Nguzo ya Dunia

Hadithi ya Dk Goodall haiwezi kutenganishwa na historia ya Tanzania yenyewe ya uhifadhi wa mazingira.

Kazi yake ya kipekee huko Gombe haijafanya tu wanyama pori kuwa maarufu Tanzania katika jukwaa la kimatifa lakini pia imedhihirisha utajiri wa aina mbalimbali ya Tanzania na ahadi yake ya kuhifadhi uzuri wa asili.

Siku yake ya miaka 90, tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Dk. Jane Goodall- mhifadhi wa kweli wa urithi wa asili wa Tanzania na kioo cha kimataifa cha uhifadhi. Urithi wake unavuka ugunduzi wa kisayansi, ukiakisi roho yake ya tumaini na harakati isiyokoma kuelekea dunia bora.


Jiunge na kampeni ya #GoodAllDay Campaign on April 3rd

Sheherekea Siku 90 ya Kuzaliwa ya Dk Jane Goodall na #GoodAllDay April 3! Jiunge na Watanzania na wafuasi ulimwenguni kote katika vitendo vya wema kuheshimu lengo lake la tumaini na wema.

Panda mti, saidia wenye uhitaji na sambaza ujumbe wa matumaini kuakisi athari chanya za Jane. Shiriki wema wako ukitumia #GoodAllDay kwenye mitandao ya kijamii ili kuhamasisha mawimbi ya utoshelevu wa kimataifa.

Tuungane kufanya siku hii kuwa sherehe ya kimataifa ya urithi wa Dk Goodall. Kuhamasisha mtandao wako kujiunga na kuonyesha ulimwengu nguvu ya wema wa pamoja.

Kama Dk Jane anavyosema, ‘Pamoja, tunaweza kufanya tofauti!’ Tukumbuke urithi wake kwa sayari na tuifanye April 3, 2024, kuwa siku ya kumbukumbu ya hatua ya tumaini la pamoja.