Majadiliano ya COP28 yadhamiria kuziwezesha jamii za asili ustawi na maendeleo

Katika harakati za kuleta mabadiliko chanya na uwezeshaji wa kifedha kwa wananchi wake, Serikali ya Tanzania imetengeneza ushirikiano wa kimkakati na taasisi za ndani na za kimataifa.

Ushirikiano huu unalenga kutengeneza uwezo wa kuingiza mapato kutokana na shughuli mbalimbali huku Carbon Tanzania ikionekana kuwa tumaini la mabadiliko chanya haswa kwa jamii za asili.

Katika ushirikiano huu, mkutano wa COP28 unaoendelea Dubai umewakutanisha viongozi wa dunia kujadili mikakati muhimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Majadiliano ya COP28 yanasisitiza umuhimu wa kupata suluhisho za kibunifu, hasa zile zinazohusisha na kunufaisha jamii za asili ikiwemo ulinzi wa mazingira.

Isack Bryson, Meneja wa Mradi wa Bonde la Yaeda-Eyasi, anaeleza alichokishuhudia katika mkutano wa COP28: “COP28 inaongelewa sana kila mahali na imeleta matumaini makubwa kwangu na jamii yangu hata kabla sijaja leo. Tunatumai kwamba kupitia kushirikishana kuhusu athari za mabadiliko ya tabinchi, njia za kukabiliana na changamoto hiyo zitatolewa hivi karibuni ulimwenguni kote kwa maisha bora na hali ya hewa inayofaa.”

Carbon Tanzania ni kampuni ya kitanzania ambayo inatekeleza   jukumu muhimu katika kuinua hali ya kiuchumi ya jamii za vijijini kupitia usimamizi endelevu wa misitu na bioanuai.

Miradi yao inazingatia kuzalisha mapato ya fidia ya kaboni inayotokana na misitu, njia ya kipekee inayowawezesha wamiliki wa rasilimali za eneo hilo haswa jamii za asili kupata mapato kwa kulinda rasilimali zao.

Huku dunia ikikabiliana na changamoto kubwa za mabadiliko ya tabianchi, jopo la COP28 linasisitiza umuhimu wa kushirikiana na jamii za asili wakati wa kuendeleza miradi inayozalisha fidia ya mapato ya bioanuai na asili.

Harakati za Carbon Tanzania zinaendana kikamilifu na mtazamo huu, zikiwasilisha mfano wa ushirikiano unaoshughulikia si tu changamoto za ikolojia bali pia kutambua na kuwezesha jamii za asili.


Kuangalia kwa undani kuhusu mikakati ya Carbon Tanzania

Mradi wa Bonde la Yaeda-Eyasi, ulioanzishwa mwaka 2012 ni uthibitisho wa faida halisi zinazofurahiwa na jamii za asilia. Ukiwa unazingatia kulinda ardhi na misitu ya jamii za wahadzabe na wafugaji wa Datooga, mradi huu uliongezwa mwaka 2021 na hivyo kuongeza mapato ya fidia ya kaboni. Hii, kwa upande mwingine, iliziwezesha jamii hizi kuajiri wafanyakazi zaidi kwa ajili ya kulinda misitu yao.

Tukiangalia kuhusu Mradi wa Bonde la Yaeda, unaonyesha kwamba zaidi ya miti 137,000 imemea vizuri, ikiwa ni ishara ya juhudi za ushirikiano. Miti hii inafanya kazi kama kinga dhidi ya ukataji miti, ikiwakilisha uthabiti wa jamii za Hadza na Datooga.

Pamoja na zaidi ya Dola za Marekani 546,912 zilizozalishwa kutokana na fidia ya kaboni, Bonde la Yaeda limekuwa msukumo wa mabadiliko makubwa katika elimu, huduma za afya, na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Ada zilizolipwa ni kwa wanafunzi 42 wa sekondari, msaada kwa watoto 558 wa shule ya msingi na msaada kwa wanafunzi watano wa chuo kikuu, zote zinatokana na mapato ya fidia za kaboni. Jumla ya Walinzi wa Misitu ya Kijiji 126 (VGS) ikiwa ni pamoja na VGS 18 wa kike, sasa ni wasimamizi wa ardhi hizi, wakifundishwa katika ulinzi wa rasilimali asilia na itifaki za ufuatiliaji. Zaidi ya faida za kifedha, eneo la Bonde la Yaeda linapata mabadiliko chanya katika hali yake ya hewa yanayotokana na juhudi za mradi huu.

Regina Safari, Mratibu wa Jamii ya Hadza, anatushirikisha mtazamo wake juu ya miradi hii: “Zaidi ya hayo, mapato ya fidia za kaboni yaliyopatikana kwa kulinda misitu yameboresha upatikanaji wa elimu kwa wengi hapa Kijiji cha Domanga, ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe. Michakato hii inafanya kazi hapa chini. Nayasihi makampuni yanayonunua fidia za kaboni kuendelea au hata kuongeza manunuzi yao. Fedha hizi ni muhimu kwa mafanikio ya mradi na ili faida zinazotolewa kwa watu binafsi na jamii ziendelee. Nawashukuru na naondoka na maneno: bila misitu, hakuna maisha.”

Mradi wa Makame Savannah ulioanzishwa mwaka 2016, unashirikiana kikamilifu na Wamasai kwa lengo la kuhifadhi mazingira muhimu ya wanyamapori. Mwaka 2022, athari za mradi zilijitokeza kupitia upatikanaji wa elimu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bweni la wasichana na malipo ya ada kwa zaidi ya wanafunzi 100 katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Faida hizi sio za kifedha tu bali zinaenda kusaidia katika kuondoa vizuizi vya asili na kuziwezesha jamii.

Supuk Olekao, Meneja wa Makame WMA, anafafanua kuhusu mabadiliko yaliyotokea: “Tulianzisha eneo la uhifadhi wa jamii au Eneo la Usimamizi wa Wanyamapori (WMA) mwaka 2009 ili kuzuia uvamizi wa ardhi yetu na ukataji miti. Hata hivyo, mamlaka ya usimamizi wa WMA ilishindwa kuutekeleza kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Tulikuwa na shirika, mawazo, na watu, lakini hatukuwa na rasilimali za kweli za kulinda ardhi na misitu yetu. Mapato ya kifedha kutokana na fidia za kaboni tunayopata sasa kwa kulinda misitu yetu kama tulivyokuwa tunafanya maana yake sasa tuna rasilimali za kuhakikisha ardhi yetu haivamiwi na misitu yetu inasimama.”


Uhifadhi wa makazi ya wanyamapori kupitia jamii

Mradi wa Milima ya Ntakata unaonyesha hadithi ya uhifadhi unaongozwa na jamii na athari zinazoweza kuonekana. Eneo la mradi ni ekari 216,000 na ndani yake kuna zaidi ya ekari 11,000 za makazi bora yanayofaa kwa Sokwe wa Mashariki wanaokaribia kupotea.

Mradi huu umekuwa kiungo muhimu katika mfumo wa ikolojia wa Greater Mahale. Zaidi ya takwimu hizo, miti milioni 1.25 iliyolindwa inaonyesha azma ya jamii za wakulima kuhifadhi makazi muhimu ya wanyama porini.

Dola za Marekani 280,922 zilizotumika kuboresha huduma na miundombinu ya afya sio tu zimeongeza ustawi bali pia zimekuwa ushuhuda wa uhusiano kati ya afya ya jamii na uhifadhi wa mazingira.

Walinzi wa Misitu wa Kijiji 55 waliopatiwa mafunzo ya ulinzi wa rasilimali asilia ni walinzi imara wa ukanda huu, wakifanya doria 150 mwaka 2022 na kuondoa mitego 14. Kama jitihada za kujenga jamii, mradi umetenga zaidi ya Dola za Marekani 221,834 kuboresha upatikanaji wa elimu.

Mradi wa Ruvuma Wilderness, ingawa bado uko katika hatua za mwanzo, unaonyesha dalili za kuridhisha. Watu wengi katika ukanda huu haswa wakulima wanashuhudia kuanzishwa kwa mradi unaolenga kuwa moja ya maeneo ya hifadhi kubwa za mipaka barani Afrika ambao utaunganisha njia za wanyama porini kati ya Msumbiji na Tanzania.


Muktadha wa COP28 katika mapinduzi ya uhifadhi

Katika muktadha wa majadiliano ya COP28, dhamira ya Carbon Tanzania ya kutoa mapato kwa uhifadhi wa asili kwa jamii za wazawa kupitia soko la kaboni la hiari inaonyesha mfano unaoweka ustawi wa jamii hizi husika mbele.

Katika majadiliano haya ya mafanikio ya pamoja, Carbon Tanzania inakuwa kama mhimili wa mabadiliko chanya, ikielezea kuhusu kuziwezesha jamii za wenyeji kushiriki katika mazungumzo ya kimataifa juu ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano unaoendelea huko Dubai unasisitiza zaidi haja ya kuendeleza miradi ambayo sio tu inazalisha mikopo ya bioanuai na asili bali pia inashirikisha na kunufaisha jamii za wazawa.

Juhudi za Carbon Tanzania zinazotolewa kupitia miradi yao ya Yaeda-Eyasi, Makame Savannah, Milima ya Ntakata na Ruvuma Wilderness zinaambatana kikamilifu na malengo yaliyotajwa katika majadiliano ya COP28.

Wakati majadiliano yanavyoendelea COP28, yakisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja na jamii za wazawa, kazi ya Carbon Tanzania inakuwa kama jambo linalogusa hisia.

Miradi hiyo sio tu inalinda mfumo muhimu wa ikolojia na makazi ya wanyama pori, lakini pia inawezesha jamii za wazawa kustawi kiuchumi na kitamaduni. Miradi hiyo inachangia sio tu kwa uhifadhi wa mazingira bali pia kwa malengo mapana ya maendeleo endelevu yanayoungwa mkono kimataifa.

Kiini cha COP28 ni kukuza ushirikiano na ubunifu ili kukabiliana kikamilifu na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Carbon Tanzania na mtazamo wake unaosukumwa na jamii, inathibitisha uwezo wake kwa mifano kama hiyo inayoshirikisha jamii. Mazungumzo yanayoendelea katika mkutano wa COP28 ni fursa ya kupaza sauti hizi na kushirikishana uelewa unaoweza kuvutia miradi kama hiyo duniani kote.

Huku mkutano wa COP28 ukivuka eneo tata la hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, hadithi ya Carbon Tanzania inakuwa kama mwanga, ikionyesha jinsi miradi iliyokita mizizi katika ushirikiano, ushiriki wa jamii na uhifadhi wa mazingira inaweza kusababisha mabadiliko chanya na ya kudumu.

Majadiliano kutoka miradi ya Yaeda-Eyasi, Makame Savannah, Milima ya Ntakata na Ruvuma Wilderness inaelezea matumaini, uthabiti na uwezeshaji ikipenya katika majadiliano ya COP28 na kuhamasisha ahadi ya pamoja kwa mustakabali endelevu na jumuishi.