Miaka 25 ya Britam Tanzania kuongoza kwa ubunifu, upatikanaji wa Bima

Dar es Salaam. Britam Insurance Tanzania katika kuadhimisha miaka 25, inaonekana kuwa kielelezo cha ubunifu katika utoaji wa huduma za bima. Ushirikiano wa kimkakati baina ya Britam na makampuni makubwa ya simu, kama Vodacom kupitia VodaBima na jukwaa la WhatsApp kupitia EazyBima, umebadilisha taswira ya bima, na kufanya iwe rahisi  kupatikana kwa wateja.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Britam, Bw. Farai Dogo, akizungumzo katika tukio la maadhimisho ya miaka 25 ya kampuni ya bima ya Britam katika soko la Tanzania alisisitiza kuwa “Upatikanaji wa huduma za bima uliowezeshwa na EazyBima ni uthibitisho thabiti wa dhamira yetu ya kuwa wabunifu katika kutoa huduma. Katika enzi hizi ambapo majukwaa ya mawasiliano yanafanya majukumu mengi katika maisha yetu ya kila siku, EazyBima inatumia ukaribu na urahisi wa WhatsApp kusaidia safari ya mteja katika kupata bima."

Akishiriki katika maadhimisho ya miaka 25 ya kampuni ya bima ya Britam, Kamishna wa Bima (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, alisema, "Serikali imeona na kutambua mchango wa Britam Insurance Tanzania, na tunona jinsi kampuni hii inavyofanya kazi kubwa katika kutatua majanga yasiyo tarajiwa.

Ushirikiano kati ya Britam na Vodacom, umewaletea suluhisho za bima mamilioni ya watu. Kwa kutumia wigo mpana wa mtandao wa Vodacom, ushirikiano huu unawezesha wateja kupata bima za magari kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi. VodaBima imekuza mchakato wa bima, kuhakikisha ulinzi unapatikana kwa  idadi kubwa ya watu.

Ubunifu wa kiteknolojia na ushirikiano wa kimkakati unadhihirisha mtazamo wa kampuni  kuelekea kukidhi mahitaji yanayobadilika ya wateja. Hasa katika enzi hizi ambapo muda ni muhimu, hatua hizi zinarahisisha na kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa bima kwa wateja.

Bw. Farai aliendelea zaidi kwa kusema "Tunapoadhimisha miaka 25 ya mafanikio ya Britam, si tu kumbukumbu ya zamani bali ni kutambua juhudi endelevu za kampuni kuendelea kuwa mbele ya mabadiliko."

Ushirikiano huu wa kiteknolojia unathibitisha dhamira ya kampuni kukutana na wateja mahali walipo. Hatua hizi ni uthibitisho wa dhamira ya Britam ya Kulinda Ndoto Zako na Kuhakikisha inakukinga  Hatari kwa miaka 25 na zaidi.
Hata hivyo Britam Kama mtoa huduma wa bima anayeaminika,  pia imejitolea kuhakikisha kwamba watu binafsi kutoka nyanja mbalimbali wanapata huduma bora za afya na huduma nyinginezo za bima. Kwa kuzingatia ujumuishi, sera za bima za Britam zinapatana na maslahi ya taifa kwa kutoa huduma ya kina. Hasa, Britam inachangia kutekelezwa kwa lengo la serikali kwa kutoa bima ya matibabu ambayo inakidhi mahitaji ya afya ya watu.