Mikakati ya Tanga UWASA katika kuboresha huduma za maji


TANGA PICS

Tanga ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania bara ambao uko Kaskazini Mashariki mwa nchi. Mkoa huu unapakana na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari ya Hindi upande wa Mashariki na mikoa ya Morogoro...

Tanga ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania bara ambao uko Kaskazini Mashariki mwa nchi. Mkoa huu unapakana na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari ya Hindi upande wa Mashariki na mikoa ya Morogoro, Manyara na Kilimanjaro upande wa Magharibi. Upande wa Kusini unapakana na Mkoa wa Pwani.

Kabla ya kukaribishwa kwa sera ya ubinafsishaji miongo miwili iliyopita, uchumi wa Tanga ulikuwa imara, ajira zilikuwa za kutosha, viwanda viliifanya Tanga ing’are. Tanga ilikuwa moja ya mikoa inayochangia pato kubwa katika bajeti ya Taifa.

Hali imeanza kurudi tena baada ya kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya Tano ambayo inaamini zaidi katika uchumi wa viwanda. Fursa mbalimbali za kiuchumi zimeanza kurejea na moja kati ya fursa hizo ni mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi eneo la Chongoleani, Tanga.

Mbali na fursa hizo, sekta mbalimbali za maendeleo sasa zimeimarika mkoani humo. Moja ya sekta ambayo imepata mafanikio makubwa ni sekta ya maji safi na usafi wa mazingira.

Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Tanga (Tanga UWASA) inaeleza kwamba, mabadiliko ya sheria ya Maji Na. 5 ya mwaka 2019 yameleta mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira mkoani humo. Mabadiliko ya sheria hiyo yameleta mapinduzi yafuatayo katika utoaji wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira Tanga:

Yameunda Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ambayo ime-chukua nafasi ya idara za maji katika halmashauri za Wilaya mbalimbali nchini. RUWASA inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wa karibu na Mamlaka za Maji.

Imefanya mgawanyo wa maeneo ya utoaji huduma kati ya Ruwasa na Mamlaka za Maji.

Sheria hii imeongeza eneo la huduma za usimamizi shughuli za majisafi na usafi wa mazingira katika baadhi ya Mamlaka ambapo katika Mkoa wa Tanga, iliyokuwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga UWASA) kuanzia mwezi Septemba 2019 imeongezewa eneo la huduma ambalo linajumuisha maeneo ya pembezoni ya Jiji la Tanga, miji ya Muheza na Pangani hivyo hivi sasa Tanga UWASA inatambulika kama Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga yaani ‘Tanga UWASA’.

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa eneo linalohudumiwa na Tanga UWASAKabla ya maeneo haya kuunganishwa, maeneo yaliyosimamiwa na Tanga UWASA ambayo ni Jiji la Tanga yalikuwa yakipata huduma ya maji kwa asilimia 97 kupitia mabomba yaliyounganishwa majumbani.

Kwa upande wa Wilaya ya Muheza upatikanaji wa maji ulifikia asilimia 35 na Wilaya ya Pangani asilimia 80 ambapo kwa kiasi kikubwa maji hayo yalikuwa yakipatikana katika vioski.

Baada ya Tanga UWASA kuunganisha eneo la kutolea huduma (kata zote 27 zinazounda Jiji la Tanga), Mji wa Muheza na Mji wa Pan-gani unaoundwa na kata nne hali ya upatikanaji wa maji kwa wananchi (House connection) imepungua kutoka asilimia 97na kufikia asilimia 89.

Kwa sasa, Tanga UWASA imeingiza maeneo ya miji ya Muheza na Pangani katika mipango yake ya utekelezaji kwa sababu ni sehemu ya eneo lake kwa mujibu wa sheria Namba 5 ya mwaka 2019.

Tunatarajia kwamba miradi mikubwa inayoendelea kujengwa katika Wilaya ya Muheza itakapokamilika itasaidia kuongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 35 na kufikia asilimia 70.

Miradi iliyotekelezwa na Serikali kuanzia mwaka 2016 imelenga kuboresha upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya mkoani Tanga.

Aidha, kuanzia kipindi hicho mpaka sasa Serikali imetenga zaidi ya Sh 10.9 bilioni kwa ajili ya kuboresha hali ya upatikanaji wa maji kupitia miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa ikiwemo Tanga Jiji, Mombo wilayani Korogwe, Horohoro wilayani Mkinga, Pangani na Songe wilayani Kilindi.

Utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali ambapo baadhi imekamilika na mingine iko katika hatua tofauti za ukamilishwaji.

Tanga Jiji

Kuna miradi miwili inayo-tekelezwa ukiwemo mradi wa uboreshaji wa mtandao wa majisafi ambapo lengo ni kuhakikisha maji yanayozalishwa yanafikia wananchi na kupunguza mivujo.

Mradi mwingine umehusisha kazi ya ulazaji wa bomba la majitaka kutoka Duga Muembeni hadi Makorora ambapo wananchi wa maeneo ya kata za Duga, Mikanjuni, Mabawa na Makorora watanufaika.

Pangani

Mradi huu umegharimu Sh681 Milioni, unalenga kuboresha miundombinu ya maji kwa kukarabati mabomba ya zamani na kuweka mapya. Mradi huu umekamilika ambapo wanufaika ni wakazi 18,700.

Mradi wa maji Mombo

Katika Mji wa Mombo kuna mgao wa maji, utekelezaji wa miradi unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika Aprili 2020 na utakapokamilika utaboresha upatikanaji wa maji na kuondoa mgawo wa maji uliopo sasa kwa wananchi.

Mradi wa maji LushotoKatika mji wa Lushoto hali ya upatikanaji wa maji ni asilimia 52 ambayo ni chini ya lengo la serikali lakini ujenzi wa mradi ambao unalenga kuwanufaisha wakazi 5,000 kazi zinaendelea. Mradi huu utakapokamilika utaongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kwenye Mji wa Lushoto na kufikia asilimia 85.

Mradi wa maji Muheza

Mji wa Muheza una tatizo kubwa la upatikanaji wa maji tayari Serikali imetenga zaidi ya Sh 6.1 Bilioni kutekeleza miradi ya upatikanaji wa maji wilayani humo. Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa maji Muheza umegharimu Sh 3.5 Bilioni, miradi hii imelenga kuongeza upatikanaji wa maji katika mji wa Muheza kutoka asilimia 35 ya sasa ili kufikia asilimia 65.

Shughuli za utekelezaji katika awamu ya kwanza zinahusisha ulazaji wa mabomba makubwa na madogo kutoka eneo la Pongwe jijini Tanga hadi Kitisa wilayani Muheza. Utakapokamilika utanufaisha wananchi zaidi ya 15,000 wanaoishi katika vijiji vilivyoko njiani vikiwemo vya Bagamoyo, Ngomeni, Tanganyika, Lusanga na Kitisa.

Awamu ya pili ya ujenzi huu ni kulaza bomba kubwa maalum kutoka chanzo cha Mowe mpaka Pongwe, lengo ni kuboresha upatikanaji wa maji Muheza, mradi utagharimu kiasi cha Sh 2.6 Bilioni na tayari utekelezaji wake umefikia asilimia 40. Awamu ya tatu ya mradi huu inalenga kujenga mradi wa maji ambao chanzo chake ni Mto Pangani.

Lengo ni kuboresha upatikanaji wa maji katika miji mitatu ya Korogwe, Muheza na Pangani. Tayari Mhandisi Mshauri ameainisha maeneo ya kuboresha na kwa sasa Serikali ipo kwenye hatua ya kutafuta mkandarasi na utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Mji wa Horohoro

Mradi wa Maji Horohoro katika Wilaya ya Mkinga unatumia chanzo kisicho salama ambacho ni bwawa la maji ya mvua. Serikali imewekeza kiasi cha fedha Sh 386 Milioni kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya maji ili kuwezesha wananchi kupata majisafi na salama karibu na makazi yao.

Mradi huu uko katika hatua za mwisho, kazi zinazofanyika kwenye utekelezaji wa mradi huo ni ujenzi wa vituo vya kusambazia maji, ukarabati wa bwawa, mtambo wa kusafisha maji ambapo wananchi zaidi ya 3,000 watanufaika.

Mji wa Songe

Mradi wa maji Songe katika Wilaya ya Kilindi unatekelezwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ya mradi huu ilikamilika mwaka 2018 na ilifanyika katika Kata ya Bokwe ambapo wananchi 5,000 wananufaika.

Awamu ya pili ya mradi huu ambao utagharimu kiasi cha Sh 1.1 Bilioni utekelezaji wake umeanza mwaka 2019 ambapo kwa sasa umefikia asilimia 45. Wananchi 15,000 wa vijiji vinavyounda kata hiyo ya Songe watanufaika. Unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili 2020.

Kwa ujumla, utekelezaji wa miradi yote hiyo umefikiwa kwa asilimia 75 na tayari Sh 5 Bilioni kati ya Sh 10 Bilioni zilizotengwa na Serikali kujenga miradi hiyo zimelipwa kwa wakandarasi na inatarajiwa kukamilika mwaka huu.

Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)

Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Tanga inahudumia maeneo ya; Muheza Vijijini, Mkinga, Pangani Vijijini, Korogwe Mjini, Korogwe Vijijini, Halmashauri ya Bumbuli, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Wilaya ya Handeni na Kilindi.

Pia kuna miradi mikubwa miwili inayoendelea kutekelezwa katika baadhi ya wilaya ukiwemo mradi wa Handeni Truck Main (HTM) ambao unasimamiwa na Mamlaka ya kitaifa ya Handeni na ule wa Jiji la Tanga unaotekelezwa na Tanga UWASA kwa ajili ya kupeleka maji mjini Muheza.

Hali ya utekelezaji wa miradi ya maji Tangu kuanza kwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya kwanza (WSDP I) mwaka 2006 hadi sasa awamu ya pili (WSDP II), Mkoa wa Tanga ume-tekeleza jumla ya miradi 79 yenye thamani ya jumla ya Sh 53,297,774,750.16 kwa mujibu wa mikataba yenye uwezo wa kuhudumia watu wapatao 424,703.Kati ya hiyo, jumla ya miradi 51 yenye thamani ya Sh 26,377,712,131/= kwa mujibu wa mikataba imekamilika na ina uwezo wa kuhudumia watu 227,640 ambapo mpaka sasa kiasi cha fedha Sh 25,216,413,942/=kimelipwa.

Miradi iliyokamilika

• Lushoto (7) - Irente, Mlalo/Mwangoi, Kivingo, Malibwi, Bumbuli, Kweminyasa na Kireti.

• Mkinga (6) - Daluni/Kibaoni, Mapatano, Kilulu, Duga, Bwagamacho, Bamba, Mwarongo na Doda.

• Muheza (8) - Ubembe, Kisiwani, Nkumba, Kibanda, Kwemhosi, Misongeni, Mikwamba na Kigongomawe.

• Pangani (7) Madanga/Jaira, Bweni, Mzambarauni, Kwakibuyu, Kigurusimba, Boza – Kimang’a, Mtangona Meka/Mseko.

• Tanga (2) – Kirare na Marungu/Geza.

• Handeni (2) – Malezi na Bwawa la maji Mkata

• Kilindi (6) Kikunde, Negero, Kwediboma, Chamtui, Kwekivu, Mafuleta.

• Korogwe- (13) Kwashemshi, Makumba, Vugiri, Mnyuzi, Mwenga, Kwamkole, Hale, Mashewa na Changalikwa, Kwamndolwa/Kwameta, Kwasemangube, Kwakombo/Kwamsisi na Mgombezi/Mgambo.

Aidha, miradi ya maji 28 yenye gharama ya jumla ya Sh 26.920 billion inaendelea kutekelezwa katika wilaya mbalimbali hadi sasa yenye uwezo wa kuhudumia wakazi 197,073 baada ya kukamilika kwake. Mpaka sasa kiasi cha Sh 14.292 billion kimeshalipwa.

Miradi inayoendelea

• Lushoto (7) - Shume/Manolo/Madala, Gologolo, Kwalei, Mgwashi, Kwang’wenda/Mbuzii, Vugana Soni Mkuzu.

• Mkinga (3) – Parungu Kasera, Mwakijembe, Mbuta.

• Muheza (5) - Mlingano, Kilongo, Umba, Mkwakwa Mafleta na Kivindo.

• Tanga (1) – Mabokweni.

• Handeni (3) - Manga, Kwandugwa na Uchimbaji wa Visima 14.

• Kilindi (3) - Jungu/Balang’a, Kwinji Muungano na Saunyi.

• Korogwe (4) – Lusanga, Mlembule, Rwengera Relini na Msambiazi.

• Pangani (1) – Mradi wa Visima 22 (utafiti wa maji aridhini, uchimbaji visima 22 na ukarabati wa visima vitatu).

Miradi inayotekelezwa kwa nguvu za ndani Jumla ya Miradi nane (8) katika Mkoa wa Tanga inatekelezwa kwa mfumo wa ‘force account’, miradi hiyo ni:

• Wilaya ya Pangani - Msaraza, Mbulizaga, Mwera-Ushongo, Mikocheni na Kibinda.

• Wilaya ya Handeni – Mradi wa maji Kwan-dugwa (miundombinu ya kusamba za maji).

• Wilaya ya Muheza – Miradi ya maji Potwe na Kwemdimu.Aidha mpaka sasa ofisi ya RUWASA Mkoa wa Tanga imepokea jumla ya Sh 782,000,000 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii. Tayari vifaa kwa ajili ya ujenzi vipo katika taratibu za manunuzi.

Miradi inayotekelezwa kupitia mpango wa malipo kwa matokeo Katika mwaka wa fedha 2019/2020

RUWASA Mkoa wa Tanga imepokea jumla ya Sh 1,157,635,818.39 kupitia mpango wa malipo kwa matokeo (PbR) kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na upanuzi wa miradi ya maji pamoja na usimamizi wake katika Wilaya zote za Mkoa wa Tanga.

Mapokezi ya fedha katika mwaka wa fedha 2019/2020

Mpaka sasa RUWASA Mkoa wa Tanga imepokea jumla ya Sh 2,114, 656,895.98 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maji kwa mchanganuo ufuatao;-

• Fedha za Malipo kwa Matokeo(PbR) – Sh. 1,157,635,818.39 jumla ya miradi 15 inaongezewa eneo la mtandao (upanuzi wa miradi) na miradi 21 inafanyiwa ukarabati itaongeza idadi ya watu 70,471 sawa na 3.1% wakazi wa Mkoa wa Tanga ukarabati na upanunzi wa miradi utakamilika March, 2020.

Miradi hii inatekelezwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Tanga

• Fedha kwa ajili ya mira-di ya ‘Force account’ – Sh. 782,000,000/=.

• Fedha kwa ajili ya Malipo ya Wakandarasi na malipo ya V.A.T – Sh. 167,021,077.59.Changamoto za sekta ya majiWakala wa Maji Vijijini -RUWASA Mkoa wa Tanga unakabiliana na changamo-to zifuatazo katika utoaji wa huduma za maji;-

Upatikanaji wa fedha zinazotumwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hazilingani na kasi halisi iliyopo sasa ya mahitaji ya fedha kutokana na utekelezaji halisi uliyofikiwa hali inayopelekea Wakandarasi kushindwa kuendelea na kazi.

Hali hii ni kutokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kuwa kubwa.Wakandarasi kuwa na uwezo mdogo wa kifedha unaosababisha kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa miradi pale malipo yao ya kazi walizofanya (hati za malipo) kuchelewa na kufanya wananchi kukosa huduma ya maji kwa wakati.

Vyanzo vya maji katika tabaka la juu ya ardhi (fresh surface water) ni haba na hata pale ambako kuna vyanzo vya aina hii uharibifu/uchafuzi ni mkubwa kwa shughuli za kibinadamu kama uchimbaji wa madini (mfano Mto Zigi).

Uelewa wa wananchi katika uchangiaji wa huduma ya maji ili miradi ya majii iwe endelevu.Uelewa mdogo wa sheria mpya Na. 5 ya mwaka 2019, hali iliyopelekea kuibuka kwa migogoro katika suala zima la uhuishaji wa jumuiya za watumia maji ili kuendana na matakwa ya sheria hiyo.

Mikakati ya RUWASA katika kuboresha huduma za maji

Pamoja na changamoto zilizopo, Mkoa umeendelea kusimamia kikamilifu na kuzishauri Wilaya katika kuweka mikakati mbalimbali kama vile;-

Kuelekeza nguvu katika miradi michache yenye matokeo ya haraka (Quick wins) na itakayokamilika mapema na kutoa huduma kwa wananchi badala ya kuwa na miradi mingi isiyokamilika kwa wakati pamoja na kutumia mfumo wa ‘force account’ ili kupunguza gharama za miradi.

Kuendelea kushirikiana na Serikali kuu kuhakikisha fedha zinapatikana na malipo ya Wakandarasi yanafanyika kwa wakati.

Kuwashirikisha wadau wa maendeleo katika kuan-daa mikakati mbalimbali ya programu za uendelevu wa miradi ya maji na usafi wa mazingira mfano‘Water, Sanitation and Hygiene’ (Wash) Program’ ili kuwezesha kuweka mifumo thabiti wa kuhakikisha uendelevu wa miradi ya maji kupitia uwekezaji katika uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji vijijini (sekta binafsi na umma kushiriki kwa pamoja katika kuwekeza na kiutendaji).