Protastructure kufungua ofisi Tanzania, haya ndiyo wahandisi wa ujenzi wanapaswa kuyafahamu

Katika hatua muhimu ya kuboresha sekta ya uhandisi nchini, Prota Software, kampuni ya Uturuki ya kutengeneza programu tumishi za kompyuta, imetangaza kufungua ofisi zake jijini Dar es Salaam, zitakazoanza kazi kuanzia Januari 2024.

Kampuni hiyo inayojulikana duniani kote kwa programu yake bora ya uhandisi wa ujenzi, ikiwa ni pamoja na ile ya Protastructure, iko tayari kuleta usanifu wa miundo ya ujenzi wa kisasa na kujenga uwezo wa uchambuzi kwa wahandisi wa ujenzi nchini. Mpango huo umewekwa wazi na Nzirorera Alexandre, Meneja Uendeshaji wa Protasoftware nchini, wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa kitaifa wa Taasisi ya Wahandisi (IET) uliofanyika jijini Arusha Novemba 30, 2023.

Wahandisi wa Kitanzania wana fursa ya kushiriki mafunzo na kupata leseni za programu ya Protastructure moja kwa moja au hata wakiwa katika maeneo ya mradi kuanzia mwezi ujao. Hatua hiyo inalenga kukidhi ongezeko la mahitaji ya bidhaa hiyo yenye uwezo usiomithilika miongoni mwa wataalamu wa uhandisi wa Tanzania. Prota Software inajijengea heshima na kuaminika maradufu kupitia utoaji wa leseni halali/halisi za Protastructure, kuendesha mafunzo ya hali ya juu na kutunuku vyeti moja kwa moja kutoka makao makuu yake nchini Uturuki.

Akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa IET, Alexandre Nzirorera alielezea shauku yake na kusema, “Ni wakati muafaka wa wahandisi wa Tanzania kupata uzoefu kamili wa suluhisho hili la uhandisi wa miundo na udhibiti tetemeko la ardhi kutoka Uturuki. Hivi sasa, tunapatikana Tanzania, tukikuhudumia ukiwa katika eneo lako la mradi moja kwa moja kutoka ofisini kwetu Dar es Salaam."

Hatua hii inaambatana na kutolewa kwa toleo la jipya la programu ya ProtaStructure Suite 2024, ambalo ni suluhisho la kimuundo la BIM lililorahisishwa kwa kuwekwa kwa pamoja vipengele na zana mpya zilizobuniwa kuleta mageuzi katika utekelezaji wa mradi na kuboresha sekta ya uhandisi kwa ujumla.

Ikiwa kama motisha ya ziada, wahandisi wa Kitanzania wanaweza kunufaika na ofa hii ya muda mfupi. Ununuzi wowote utakaofanywa au kuwekewa nafasi na Watanzania kabla ya wiki hii kuisha utapata punguzo la asilimia 40, kama ilivyobainishwa kwenye mkutano wa kitaifa wa wahandisi.

Upanuzi wa kimkakati wa ProtaSoftware nchini unalenga kuanzisha enzi mpya ya uvumbuzi na utaalamu, kuzalisha wahandisi katika ukanda wa Afrika huku wakiwa na fursa isiyo na kifani ya kuleta masuluhisho yenye kutumia teknolojia ya kisasa na mafunzo. Mustakabali wa uhandisi nchini unapitia mageuzi kikamilifu na programu za Prota kwa ubora na teknolojia ya kisasa.


Furahia vipengele vipya vya programu ya ProtaStructure Suite 2024

ProtaStructure Suite 2024 inaleta katika soko maarifa mapya ili kusaidia wahandisi wa miundo ya ujenzi katika shughuli zao za kila siku. Kuanzia mbinu za ubunifu wa miundo kwa vitendo hadi teknolojia mpya za muundo, programu hii ina kila kitu unachohitaji ili kuifanya miradi yako kuwa ya viwango vya juu zaidi. Kwa zaidi ya miaka 35 ya uzoefu, Prota Software inajivunia kuendelea kuleta toleo jipya na bora zaidi la programu za ProtaStructure Suite.

Uundaji na usanifu umeboreshwa maradufu

Kiolesura cha mtumiaji cha programu ya ProtaStructure Suite 2024 kimebuniwa kwa kumfikiria mhandisi mwenyewe, na hivyo kupunguza muda unaotumika katika utekelezaji wa mradi. Vipengele vipya ni pamoja na:

  • Composite Slab Design
  • Automated Rebar Layout for Arbitrary Corewalls
  • Tie Beams in Foundation


Uundaji na uhamishaji miundo umekuwa wa vitendo zaidi

Wepesi, uharaka na ufanisi wa ubunifu wa muundo unaopatikana katika programu ya ProtaStructure umevutia wahandisi wengi ulimwenguni kote kufikia sasa. Kupitia ProtaStructure Suite 2024, tunalenga kuboresha mvuto huu uliopo sasa kwa zana na vipengele bora zaidi. Hebu tukupitishe katika vipengele vipya muhimu ambavyo vitachangia uundaji wako wa muundo kuwa bora na ProtaStructure sasa!

Utengenezaji misingi katika miinuko tofauti (hatua za utengenezaji misingi)

• Chemchemi za mlalo katika muundo wa msingi

• Uunganishwaji wa vitalu vinavyofanana.


Misimbo mipya ya usanifu imeanzishwa

ProtaStructure Suite 2024 inawezesha usanifu wa aina mbalimbali na misimbo ya matetemeko, inayowaruhusu wahandisi kuunda, kuchanganua, kusanifu na kufafanua miundo kulingana na misimbo wanayopendelea. Misimbo mipya iliyoletwa katika toleo hili ni pamoja na:

• Msimbo wa Seismic wa Kolombia (NSR10-A)

• Msimbo wa Kihindi wa Seismic (IS 1893).


Misimbo ya matetemeko iliyoiboreshwa

ProtaStructure Suite 2024 imetambuilisha misimbo mipya ya matetemeko iliyoboreshwa ili kuwasaidia wahandisi kubuni majengo salama katika maeneo yanayokumbwa na matetemeko ya ardhi. Vipengele vipya ni pamoja na:

• Nonlinear seismic isolators

•User-defined periods in EQS analysis

•Members not part of lateral system (vertical-only).


Muunganisho unaoongoza wa mfumo wa BIM

ProtaStructure Suite 2024 inaleta sokoni muunganisho unaaongoza katika sekta ya uhandisi wa mfumo wa BIM na viungo vya pande mbili katika majukwaa mengine makuu ya mfumo wa BIM. Maboresho mapya yanahusisha pamoja na:

Updated seamless IFC communication

•Pad footings and pile caps communicated with Autodesk Revit

•Improved analytical links with ETABS

Nziza Global LLC kama kituo cha uendeshaji wa mafunzo ya Protastructure nchini tayari imeanzisha ofisi hizo Dar Es Salaam, Dar Es Salaam, Ghorofa ya Pili ya jengo la DERM PLAZA na iko wazi kwa biashara kuanzia Januari 01, 2024. Huduma kituoni zinapatikana kwa simu + 255 752 303 123 au barua pepe kwa [email protected]