Salamu za Mwaka Mpya za Balozi wa China nchini Tanzania

Muda unavyokwenda haraka! Mwaka 2024 unakuja kama ilivyopangwa. Kwa niaba ya Ubalozi wa China nchini Tanzania, napenda kutoa salamu zetu za dhati na kuwatakia heri ya mwaka mpya Wachina wenzangu wote wanaofanya kazi, kusoma na kuishi Tanzania. Shukrani zangu pia ziende kwa marafiki ambao wamejitolea na kuunga mkono urafiki wa China na Tanzania.

Mwaka 2023 ni wa muhimu sana kwa China inapoendelea kutafuta maendeleo. Katika hatua mpya ya kuanzia, nchi imepata maendeleo thabiti katika maendeleo yenye ubora wa hali ya juu na viwango vya hali ya juu katika ufunguaji wa milango.

Uchumi wake unakadiriwa kukua kwa 5.4%, na mchango wake katika ukuaji wa uchumi duniani utazidi 30%, ukiendelea kuwa mstari wa mbele miongoni mwa uchumi mkubwa. Hatua madhubuti zimechukuliwa katika kuijenga China kuwa nchi yenye ubunifu. Uchunguzi wa Tianwen-1 kwenye sayari ya Mirihi ulitua na kuchunguza sayari hiyo katika kile kilichokuwa ujumbe wa kwanza wa China wa kutafiti Mirihi. Wanaanga wa China wameingia kwenye kituo cha anga za juu cha China, na C919, ndege kubwa ya abiria ambayo China ilijitengenezea, ilikamilisha uzinduzi wa safari yake ya kwanza ya kibiashara.

Diplomasia ya mkuu wa nchi imekuwa ikitoa mwongozo katika diplomasia kuu ya China. Mwaka  2023 ni kumbukumbu ya miaka 10 ya pendekezo la Rais Xi Jinping kwa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na Mpango wa Ukanda na Njia. Miezi miwili tu iliyopita, Kongamano la tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda na Njia lililofanyika Beijing na lilipata washiriki kutoka zaidi ya nchi 150 na mashirika 40 ya kimataifa, wote wakikutana kwa pamoja kutambua muongo mmoja wa jitihada hii muhimu.

Sasa, mpango huo umesimama kama jukwaa kubwa zaidi la ushirikiano wa kimataifa, na pia manufaa ya umma inayokubaliwa zaidi kote ulimwenguni. Ukuaji thabiti wa China unatoa mwanga wa imani na nguvu kwa ulimwengu wenye changamoto, na kutoa mchango mkubwa kwa amani na maendeleo ya kimataifa.

Mwaka 2023 umekuwa wa maajabu makubwa kwa uhusiano wa China na Tanzania. Kama nchi ya Kiafrika yenye umuhimu mkubwa, Tanzania ina jukumu muhimu katika uhusiano wa China na Afrika. Ni kipaumbele cha kidiplomasia cha China kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na Tanzania. Mwaka 2023, pamoja na marafiki kutoka maeneo yote ya jamii nchini Tanzania, tuliadhimisha miaka 74 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na maadhimisho ya miaka 10 ya ziara ya Rais Xi nchini Tanzania na pendekezo la kanuni za uaminifu, matokeo halisi, mshikamano , na nia njema na kwa Mpango wa Ukanda na Njia.

MHE. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mara nyingine alikutana na MHE. Rais Xi mjini Johannesburg Agosti, 2023, ikiwa ni tangu ziara yake ya mafanikio nchini China mwaka 2022. Hii inaonyesha uaminifu wa hali ya juu wa kisiasa kati ya mataifa hayo mawili. Kwa kuongozwa na marais wote wawili, China na Tanzania zinaweza kuwa ni kielelezo cha uhusiano kati ya China na Afrika na ushirikiano wa Kusini-Kusini huku zikiendelea kujitolea kuwa na ushirikiano wenye nguvu zaidi wa kimkakati na ushirikiano.

Kwa muda wote wa 2023, China ilibaki kuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Tanzania na mwekezaji mkubwa zaidi. Kuanzia Januari hadi Novemba, biashara baina ya nchi hizo mbili ilifikia dola za Marekani bilioni 7.96, ikiwa ni ongezeko la 6.8% la mwaka hadi mwaka. China iliondoa ushuru wa asilimia 98 ya bidhaa za Tanzania zinazouzwa China kwenda China, na kuruhusu bidhaa zake za kilimo bora kama parachichi na vyakula vya baharini kutoka vyanzo halisi vya samaki kuingia katika soko la China. Kwa hivyo, China inatarajiwa kudumisha hadhi yake kama mshirika mkuu wa biashara wa Tanzania kwa mwaka wa nane mfululizo.

Zaidi ya hayo, maendeleo makubwa yamepatikana katika eneo la uwekezaji. Ushahidi wa hilo ni USD311 milioni zimewekezwa katika Kiwanda cha Kioo cha Wangkang Sapphire Float Glass. Kupitia ubia huo, wafanyabiashara wa China wanachangia kikamilifu katika uboreshaji wa viwanda na kilimo nchini Tanzania. Hii sio tu inatengeneza ajira lakini pia huleta faida dhahiri kwa wenyeji.

Mwaka 2024 ni muhimu kwa China kutekeleza Mpango wake wa 14 wa Miaka Mitano. Tutaadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania. Katika Mkutano wake Mkuu wa Kazi ya Kiuchumi uliofanyika mwezi uliopita, Chama cha Kikomunisti cha China kilielezea mipango ya ufunguaji milango wa kiwango cha juu. Huku tukichukua hatua kuu nane ili kuunga mkono harakati zetu za pamoja za ushirikiano wa hali ya juu wa Ukanda na Njia, tutaratibu utekelezaji wa miradi ya kihistoria na miradi "midogo lakini mizuri" ya kujikimu.

Juhudi hizi zitaleta fursa zaidi kwa maendeleo ya Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Mwaka 2024, China itasimama tayari kuchangia maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania kama fursa ya kurejesha urafiki wa jadi na kukabiliana na changamoto kwa pamoja kwa ajili ya ustawi wa pamoja. Juhudi hizi za pamoja zinalenga kuisaidia Tanzania katika kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya 2025 na mpango wake wa tatu wa miaka mitano.

Mwaka mpya unapoanza, kila kitu huchukua sura mpya. Mwaka ujao utaashiria Mwaka wa Dragoni katika kalenda ya mwezi ya Kichina. Dragoni inawakilisha ishara iliyokita mizizi katika roho ya kitaifa ya China. Kama watu wasemavyo, "Kukiwa na dragoni angani na chui katika miondoko, ustawi wa taifa ni wa uhakika".

Tunazitakia China na Tanzania mafanikio makubwa na watu wetu maisha bora. Mahusiano kati ya mataifa haya mawili yasonge mbele kwa kasi. Kwa marafiki zetu wote, ninawatakia kazi njema, familia zenu zijazwe na furaha, na kuwa na Mwaka Mpya wa furaha.