Ushiriki wa Repoa katika mnyororo wa thamani kuongeza uzalishaji, upanuzi wa viwanda na biashara

Muktasari:

  • Ushiriki katika minyororo ya thamani ya kikanda na kimataifa unaweza kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya upanuzi wa viwanda na biashara.

Maana halisi ya uwezo wa uzalishaji na ukuaji wa uzalishaji kutoka kwenye mashirika/taasisi husika za kimataifa:


Michakato ya kukuza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya upanuzi wa viwanda na biashara

Uwezo wa uzalishaji hukua ndani ya nchi kupitia michakato minne yenye uhusiano wa karibu: utafutaji na kukuza mitaji, maendeleo ya kiteknolojia, usimamizi na mabadiliko ya kimuundo.


Kuelekea mafanikio ya juu ya uzalishaji—ahadi ya ushiriki katika minyororo ya thamani ya kikanda na kimataifa

Ushiriki mkubwa katika minyororo ya thamani ya kimataifa na kikanda— yaani ushiriki wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja unaohusishwa na kuongezeka kwa mauzo ya nje na ndani ya bidhaa za kati—, huleta athari za moja kwa moja katika uchumi. Athari chanya ni kubwa zaidi kwa nchi ambazo ziko mbele katika viwango vya juu vya uzalishaji. Kushiriki katika minyororo ya thamani ya kimataifa na

Nchi kadhaa—Lesotho, Eswatini (zamani Swaziland), Tanzania, na Mauritania (kwa utaratibu huo)—zina fursa kubwa zaidi za kupata (bidhaa zinazoagizwa kutoka nje zinazotumiwa kuzalisha bidhaa za kati au za mwisho kwa ajili ya kuuza nje zilizoongezewa thamani) hasa kwa kuzingatia wingi wao wa fursa za uagizaji wa bidhaa za nje ya nchi katika sekta ya wiwanda vya nguo. Mataifa haya na mengine kadhaa yameweza kushiriki katika minyororo ya thamani ya kimataifa ya utengenezaji wa nguo kwa sababu ya faida ya upendeleo wa kibiashara—hususan Mpango wa Marekani wa Ukuzaji Uchumi Afrika (AGOA)—ambao ni wa kipekee kwa Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hivi majuzi, nchi kadhaa za Afrika Mashariki (ikiwa ni pamoja na Ethiopia, Kenya, na Tanzania) zimeimarisha ushiriki wao katika minyororo ya thamani ya kimataifa katika viwanda vya bidhaa za kilimo na mauzo ya nje ya bidhaa—ikiashiria fursa ya kushiriki katika minyororo ya thamani ya kimataifa kwa nchi nyingine zilizomo ndani ya ukanda huo.

Hivyo, kukuza ushiriki katika minyororo ya thamani ya kimataifa na kikanda ni sera ambayo Tanzania na watunga sera wa nchi nyingine zinazoendelea wanapaswa kuzingatia kama nyenzo ya kuongeza uwezo wa uzalishaji mali kupitia utafutaji mitaji, uhawilishaji wa teknolojia, na ufikiaji mpana wa masoko ya kikanda na kimataifa. Haya ni muhimu kwa mafanikio endelevu ya mkakati wa ukuaji unaoongozwa na mauzo ya nje wa nchi.


Ahadi ya kibiashara kwa huduma katika kuimarisha ushiriki katika minyororo ya thamani ya kikanda na kimataifa

Huduma ni kiunganishi muhimu katika kuwezesha ununuzi na uuzaji na uendeshaji wa biashara, na katika kuunganisha wazalishaji na walaji kupitia minyororo ya thamani ya kimataifa na kikanda pamoja na kutumika kama zana muhimu katika michakato ya uzalishaji. Huduma kama vile fedha, usafiri, nishati, mawasiliano ya simu, msaada wa kisheria, na usambazaji, huongeza tija katika uzalishaji, bidhaa na uchumi kwa jumla—na, kwa kufanya hivyo, huboresha hali ya ushindani na uchumi wa nchi ikilinganishwa na dunia nzima. Huduma pia husaidia kuhawilisha ubunifu wa uzalishaji na kuendea kwa teknolojia. Ushindani wa kampuni za uzalishaji hutegemea, kwa kiasi fulani, upatikanaji wa huduma za wazalishaji wa bei ya chini, huduma za uzalishaji wa ubora wa hali ya juu— ikiwamo mawasiliano ya simu, usafiri na usambazaji huduma—na vilevile huduma za kifedha za kati. Hivyo, huduma ni zana muhimu katika biashara ya bidhaa—na huo ndiyo ni ushiriki wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja katika minyororo ya juu ya thamani ya kimataifa na kikanda.

Hata hivyo, huduma kama hizo zinasaidia uchumi kwa ujumla na ushiriki wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja katika minyororo ya juu ya thamani ya kimataifa na kikanda kwa njia kadhaa zifuatazo:

Kwa jumla, uwezo wa kampuni kushiriki kikamilifu katika minyororo ya juu ya thamani ya kimataifa na kikanda pia inategemea na upatikanaji wa huduma wa mawasiliano ya simu, usafiri, huduma za kifedha, na huduma nyingine za biashara kama vile uhasibu na huduma za kisheria. Bila kusahau kwamba, kinyume chake, huduma za gharama ya juu, zenye ubora duni, hugeuka kuwa kama “kodi” kwa wafanyabiashara na hususan wale wanaouza bidhaa nje ya nchi. Hivyo, huduma ni nyenzo muhimu katika biashara ya bidhaa.


Maarifa kwa watunga sera yenye lengo la kuimarisha uwezo wa uzalishaji

ya thamani ya kimataifa na kikanda zinaweza kufanya yafuatayo:


Hitimisho na mapendekezo ya kisera

Kuimarishwa kwa uwezo wa uzalishaji wa nchi kunajumuisha fursa ya upanuzi wa viwanda na biashara na ushiriki mzuri katika minyororo ya thamani ya kikanda na kimataifa. Rasilimali za uzalishaji, uwezo wa ujasiriamali na mahusiano ya uzalishaji hutengenezwa na kupitia mabadiliko baada ya muda fulani kupita, pamoja na mambo mengine, ushiriki mzuri wa nchi katika minyororo ya thamani ya kikanda na kimataifa. Hili linapotokea kwa uendelevu, uwezo wa uzalishaji wa uchumi pia unaimarishwa kwa njia endelevu, hivyo kufanya ukuaji wa uchumi, upanuzi wa viwanda na biashara kufanikiwa na kuwa  endelevu.

Inapendekezwa kuwa mfumo huu wa uchambuzi utumike ili kuwafahamisha wachambuzi wa sera, watendaji wa sekta binafsi, na wafanya maamuzi katika taasisi za umma zinazohusika na kukuza uchumi, maendeleo ya viwanda, uwekezaji, upanuzi wa biashara na maendeleo ya sekta binafsi.

Liko ndani ya uwezo wa wahusika hawa, kushughulikia ipasavyo vikwazo mbalimbali vya ukuaji wa uzalishaji ili Tanzania iendeleze kasi yake ya ukuaji, kufikia uwezo wake wa hatua za kimaendeleo, kudumisha ushindani katika soko la kikanda na kimataifa, na kufanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa umaskini.


Imeandikwa na Ahmed Ndyeshobola, Donald Mmari