Utamaduni na historia kubwa ya Japan na Tanzania

   Mtukufu Mfalme na Mtukufu Malkia wa Japan.

Muktasari:

Siku ya Kuzaliwa ya Mfalme ni sikukuu ya kitaifa katika kalenda ya Kijapani inayosherehekewa siku ya kuzaliwa kwa Mfalme anayetawala, ambayo kwa sasa ni Februari 23, kwani Mtukufu Mfalme wa 126 Naruhito alizaliwa siku hiyo mnamo 1960. Enzi mpya ya utawala wa “Reiwa” chini ya Mtukufu Mfalme ilianza tarehe 1 Mei 2019.

Siku ya Kuzaliwa ya Mfalme ni sikukuu ya kitaifa katika kalenda ya Kijapani inayosherehekewa siku ya kuzaliwa kwa Mfalme anayetawala, ambayo kwa sasa ni Februari 23, kwani Mtukufu Mfalme wa 126 Naruhito alizaliwa siku hiyo mnamo 1960. Enzi mpya ya utawala wa “Reiwa” chini ya Mtukufu Mfalme ilianza tarehe 1 Mei 2019.

Tarehe 22 Oktoba 2019, washiriki wa familia ya kifalme na viongozi wengine wa kimataifa kutoka kote ulimwenguni walihudhuria “Sokui no Rei”, Sherehe ya Kutawazwa.

Tanzania iliwakil-ishwa vyema sana na Mheshimiwa Kapteni Mstaafu George Huruma Mkuchika (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais. Wanafamilia wa Ufalme wa Japan wametembelea Tanzania na wanathamini kumbukumbu za nchi hii nzuri yenye utajiri wa mila na desturi.

Mfalme Mstaafu na Mke wa Mfalme Mstaafu, Wazazi wa Mtukufu Mfalme wa sasa bado wanakumbuka safari yao Tanzania ya mwaka 1983. Ilikuwa heshima kwao kujifunza toka kwa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Nyerere juu ya utajiri wa lugha ya Kiswahili na misamiati yake.

Mwana Mfalme, Binti Mfalme Akishino na familia yao.

Mwezi Julai mwaka 2014, wanaufalme Fumihito na mkewe Kiko Akishino walitembelea Tanzania na kuvutiwa sana na watu na asili ya nchi hii. Tangu kuanza kipindi cha utawala wa Reiwa, wanaufalme hawa wamepanda hadhi ya kuwa warithi wa kiti cha ufalme, na sherehe za kutangazwa kwa mrithi wa kiti cha ufalme zilifanyika tarehe 8 Novemba, 2020. Mtoto wao wa kwanza wa kiume, Mwanaufalme mrithi Hisahito anahudhuria masomo katika shule ya sekondari ya chuo kikuu cha Ochanomizu.

Japan na Tanzania

Kwa Japan, Tanzania kijiografia ni miongoni mwa nchi zilizo karibu zaidi katika bara la Afrika na Wajapani wengi wanahisi kuwa karibu zaidi na mioyo yao. Wema na uchangamfu wa Watanzania ni sawa na wa watu wa Japan.

Leo, tukiadhimisha siku ya kitaifa ya Japan, tuitazame Japan na uhusiano wake wa kirafiki na Tanzania kwa miaka sitini.

Japan inaunga mkono juhudi za ujenzi wa taifa la Tanzania kwa namna inayoheshimu umiliki wa Tanzania kupitia majadiliano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuzingatia misingi ya Usalama wa Binadamu yenye dhana kuu ya “kutomwacha mtu nyuma.”

Tangu mwaka 1962, Serikali ya Japan imetekeleza ushirikiano wa kimaendeleo katika nyanja mbalimbali ambao umechangia kwa kiasi kikubwa kujenga amani, utulivu na ustawi wa Tanzania.

Kiasi cha Msaada Rasmi wa Maendeleo (ODA) kimekusanywa na kufikia JPY bilioni 350 (Tsh trilioni 70) kwa miongo kadhaa na kuifanya Tanzania kuwa nchi inayonufaika zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Hafla ya uzinduzi wa barabara mpya ya Bagamoyo awamu ya pili kutoka kulia kwenda kushoto: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Balozi wa Japan, Shinichi Goto, Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Naofumi Yamamura, Mwakilishi Mkuu wa Ofisi ya JICA Tanzania

Maeneo yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na miundombinu, ujenzi wa viwanda na uboreshaji wa utumishi wa umma. Eneo la kijiografia la Dar es Salaam linairuhusu kuchukua nafasi kubwa katika kuunganisha nchi nyingine jirani na Bahari ya Hindi na Pasifiki.

Kwa hivyo, kuboresha uwezo wa usafiri katika jiji la Dar es Salaam kunamaanisha kuleta ukuaji wa haraka wa uchumi sio tu kwa Tanzania bali pia kwa nchi zingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko.

Mnamo Desemba 2021, hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Upanuzi wa Barabara Mpya ya Bagamoyo (Awamu ya 2), kip-ande cha Mwenge-Morocco ilifanyika na kuhudhuriwa na Mhesimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi.

Mradi huu utakuwa mfano wa miundombinu ya barabara yenye ubora wa juu. Mapema mwezi huu, Japan ilisaini miradi miwili ya mkopo ya ODA ambayo ni Mradi wa Uboreshaji wa Barabara ya Arusha-Holili (Yen bilioni 24.310 takriban TZS bilioni 492) na Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji Mijini Zanzibar (Yen bilioni 10.864 = TZS bilioni 221) pamoja na msaada mmoja wa ruzuku, mradi wa Ukarabati wa Bandari ya Kigoma (Yen bilioni 2.726 takriban TZS bilioni 55).

Miradi hii mitatu ni sehemu ya ahadi za TICAD7, inayoonyesha dhamira kamili ya Japan ya kuchangia katika uwekezaji katika miundombinu bora ili kuimarisha uunganishaji, Usalama wa Binadamu na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Mwelekeo mpya wa mahusiano ya nchi mbiliKatika miaka sitini ya urafiki, Japan inatazamia kuboresha zaidi uhusiano na Tanzania. Katika hili, Mkutano wa nane wa kimataifa wa Tokyo kwa maendeleo ya Afrika (TICAD8) unaotarajiwa kufanyika Tunisia mwaka huu ni muhimu sana.

Ukitazama mafan-ikio yake ya kihistoria kwa zaidi ya robo karne, TICAD inaendelea kuwa muhimu zaidi katika ngazi ya mikutano ambayo inaleta pamoja wadau wote kujadili masuala ya maendeleo ya Afrika.

Teknolojia mpya kama vile fedha za mitandaoni na miamala ya fedha ya kimtandao kwa mfano wa namna chanya ambayo teknlojia imebadilisha uchumi na kuzalisha fursa za ajira kwenye eneo la Afrika. Hasa, UVIKO-19 imefichua udhaifu wa Afrika ikiwa ni pamoja na katika nyanja ya sekta za afya na matibabu.

Mabadiliko ya kidijitali ya jamii, yaliyoharakishwa kupitia janga hili, yanapaswa pia kujumuisha nchi za Kiafrika. Kando na hayo, ni muhimu kushughulikia masuala ya mazingira ya kimataifa kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na mazungumzo ya bioanuwai, ambayo hakuna nchi moja inaweza kukabiliana nayo peke yake.

Kwa kuangazia sio tu changamoto zilizotajwa hapo juu lakini pia kuzingatia uwezekano wa maendeleo kama vile kukuza uchumi wa kidijitali, Japan itaendelea kusaidia maendeleo yanayoongozwa na Waafrika kupitia watu, teknolo-jia na uvumbuzi. TICAD8 ita-toa fursa nyingi kwetu kujadili masuala haya yote kuelekea siku zijazo nzuri.