Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamanda Muliro: Mazingira safi ni nguzo ya usalama wa Taifa

Muktasari:

  • Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa yanaendelea katika Viwanja vya Sabasaba, taasisi mbalimbali zinaendelea kuelimisha wananchi kuhusu huduma na shughuli wanazozitoa, ikiwemo uhifadhi na usimamizi wa mazingira.

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema usafi wa mazingira ni nguzo muhimu ya ulinzi na usalama wa Taifa, akibainisha kuwa mazingira bora yanachangia kulinda afya ya wananchi, kuimarisha utulivu wa jamii na kuchochea maendeleo ya uchumi.

Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Julai 8, 2026 alipotembelea Kijiji cha Mazingira cha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam.

Amesema mazingira machafu huchochea kuenea kwa magonjwa, huongeza hatari ya mafuriko, huharibu miundombinu na yanaweza kusababisha changamoto za kijamii na kiusalama, hivyo usafi wa mazingira unapaswa kuwa sehemu ya utamaduni wa kila Mtanzania.

"Usafi wa mazingira si jukumu la Serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mwananchi. Tukitunza mazingira yetu tunalinda afya, maisha na usalama wa Taifa," amesema Muliro.

Amewataka wananchi, taasisi za umma na binafsi, viongozi wa serikali za mitaa pamoja na wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika shughuli za usafi wa mazingira, kuhifadhi mazingira na kutekeleza sheria zinazosimamia sekta hiyo ili kujenga Taifa lenye afya na maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, NEMC imesema ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi za Serikali na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha mazingira yanaendelea kuhifadhiwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Baraza hilo limeendelea kuhimiza wananchi kusimamia ipasavyo taka, kudhibiti uchafuzi wa mazingira, kulinda vyanzo vya maji, kupanda na kutunza miti pamoja na kuzingatia matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

Kwa mujibu wa NEMC, hatua hizo zitasaidia kuboresha afya ya jamii, kuongeza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuharakisha maendeleo endelevu ya Taifa.

Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa yanaendelea katika Viwanja vya Sabasaba, taasisi mbalimbali zinaendelea kuelimisha wananchi kuhusu huduma na shughuli wanazozitoa, ikiwemo uhifadhi na usimamizi wa mazingira.