Makonda aongoza kura za ubunge Arusha Mjini
Arusha. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameongoza kura za maoni katika nafasi ya ubunge Jimbo la Arusha Mjini kwa kupata kura 9,056.
Makonda na wenzake sita walikuwa wakiwania nafasi kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi( CCM), katika jimbo hilo ambalo lilikuwa likiongozwa na Mrisho Gambo.
Matokeo hayo yametangazwa leo Jumatatu Agosti 4,2025 na Mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha, Timothy Sanga amesema jumla ya wajumbe ilikuwa ni 10,186 ila waliopiga kura ni 9,276.
Wengine na matokeo yao kwenye mabano ni Mustapha Nassoro (83),Hussein Gonga (46),Ally Babu (28),Aminatha Toure (26),Lwembo Mghweno (16) na Jasper Kishumbua (10).