Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwakitinya: Samia amewawezesha vijana na kinamama, tuendelee kumpa dhamana

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara, Mussa Mwakitinya, amepongeza juhudi za maofisa usafirishaji, maarufu bodaboda kwa kuendelea kuimarisha amani, akiwasisitiza kuipiga kura nyingi CCM ifikapo Oktoba 29,2025.

Mwakitinya yupo katika ziara mkoani Geita yenye lengo la kumtafutia kura za kishindo mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan.

Alisema dhima ya uwepo wa Ilani ya CCM ni kutekeleza ahadi zake ikiwemo kujikita katika kuongeza ajira kwa vijana, kukuza kipato na kuondoa umasikini.

Alisema Samia ametoa kiasi cha Sh124 milioni kwa ajili ya mikopo ya pikipiki wilayani humo, hatua inayosaidia kuongeza ajira zisizo rasmi na kuinua kipato cha vijana.

Aidha, aligusia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 iliyokuwa imeahidi kuleta ajira milioni nane, ambapo hadi kufikia mwaka 2025, Rasi Samia alikuwa amefanikiwa kutoa ajira milioni 8,08,203.

Alifafanua Samia ametoa Sh99 bilioni kwa ajili ya mikopo ya kinamama kwa sababu wanalea familia, watoto kinababa na jamii kwa ujumla.

“Naomba kabla hujaanza shughuli zako nenda kapige kura kwani ndiyo itakupa haki ya kuhoji maendeleo katika eneo lako. Usipopiga kura utakosa uhalali wa kuhoji kwa sababu hujaweka huo uongozi kwenye maeneo yako.”

“Mkapige kura tuendelee kuongeza uchumi na kuleta ajira kwa vijana, nimekuja kuomba kura za Samia, Dk Doto Biteko na diwani. Naombeni kura hizi tatu kwa ajili ya maendeleo ya Mbogwe,”alisema Mwakitinya akiwa wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Akifafanua zaidi amesema Rais Samia ameahidi kuwapatia wananchi mikopo isiyokuwa na riba kwa ajili ya kinamama na vijana akisaidiwa na mwanaye mgombea wa Jimbo la Mbogwe, Dk Doto Biteko.

“Viongozi hawa hawapendi kuwaona Watanzania wakiumizwa na mikopo kausha damu ndiyo maana Samia akatenga kiasi hicho cha fedha.”

Alisema kama ambavyo ilani ya CCM ilivyoelekeza   kukuza uchumi wa Mtanzania na kuongeza ustawi wa jamii, ndicho kinachokwenda kufanywa na Rais Samia akipata kura za kishindo na kusalia madarakani.

 “Rais anawapenda vijana wa Tanzania na ndiyo maana ametenga mafungu ya fedha maalumu kwa ajili ya kuwakopesha mikopo nafuu,”alisema.