Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenda ataja mkakati mpya wa kuongeza mapato ya kodi

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Yusuph Mwenda, akizungumza mkutano wa utendaji kazi wa TRA kwa mwaka wa fedha 2025/26 na mikakati ya 26/27 ni ya TRA nchi nzima mkoani Arusha.

Muktasari:

  • Mwenda amesema mafanikio hayo yanaonyesha kuwa kuimarisha ushirikiano na kujenga mazingira rafiki kwa walipakodi ni miongoni mwa nguzo muhimu za kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema itaendelea kuimarisha ulipaji wa kodi kwa hiari kwa kusimamia na kukusanya kodi kwa haki na weledi, sambamba na kutekeleza maelekezo ya Rais kuhusu kujenga imani ya walipakodi.

Akizungumza leo, Jumatatu Julai 6, 2026 Jijini Arusha, katika kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa TRA kwa mwaka wa fedha 2025/26, Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph  Mwenda amesema mamlaka hiyo imejipanga kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya TRA na utoaji wa Tuzo za Rais yaliyofanyika Julai 1 mwaka huu.

Mwenda amesema TRA itaendelea kuwaheshimu walipakodi wote huku ikichukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokwepa kulipa kodi, akisisitiza kuwa hatua hizo zitachukuliwa kwa kuzingatia sheria na heshima.

"Hatutakuwa na kodi ya dhuluma. Walipakodi hawapaswi kuihujumu nchi kwa kukwepa kulipa kodi, na kwa upande mwingine TRA haitawadhulumu walipakodi kwa kufanya makadirio yasiyo sahihi ya kodi," amesema.

Amesema ili kuongeza ulipaji wa kodi kwa hiari ni muhimu kujenga uaminifu kati ya TRA na walipakodi kupitia usimamizi wa haki wa kodi, matumizi yenye uwajibikaji ya mapato yanayokusanywa na Serikali pamoja na kuboresha huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo ili kurahisisha biashara na ulipaji wa kodi.

Kwa mujibu wa Mwenda, ushirikiano uliopo kati ya TRA na walipakodi umechangia mafanikio makubwa ya ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Ameeleza kuwa makusanyo ya kodi yameongezeka kutoka takribani Sh21 trilioni kwa mwaka wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani hadi kufikia Sh37.96 trilioni, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 77.

Mwenda amesema mafanikio hayo yanaonyesha kuwa kuimarisha ushirikiano na kujenga mazingira rafiki kwa walipakodi ni miongoni mwa nguzo muhimu za kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi.