Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Mbeya ataja sababu zinazokwamisha upatikanaji wa thamani ya fedha

Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali  nchini za ununuzi walio shiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa matumizi ya Mfumo mpya  wa NeST yaliyo fanyika katika ukumbi wa City Peack  jijini Mbeya. Picha na Hawa Mathias

Muktasari:

  • Agizo hilo amelitoa leo Jumatatu Desemba 15,2025,wakati akifungua mafunzo kwa Taasisi za Umma juu ya Matumizi ya Mfumo wa Kieletroniki wa Manunuzi (NeST), sambamba na moduli mpya yaliyofanyika katika ukumbi wa City Peack Jiji la Mbeya.

Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya(RC), Beno Malisa ametaja moja ya sababu zinazo kwamisha upatikanaji wa thamani ya fedha ni pamoja na usimamizi hafifu wa mikataba ya ununuzi wa umma.

Katika hatua nyingine Malisa,  ameagiza watumishi wa Ofisi za Umma nchini kutumia mfumo huo  kuhakikisha suala la  ununuzi wa umma linakwenda kuzingatia uwazi,uwajibikaji, haki na kuongeza ufanisi sehemu za kazi.

 Malisa, ametoa kauli hiyo leo  Jumatatu  Desemba 15,2025 ,wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa  Kieletroniki wa  manunuzi ya Umma (NeST),yakihusisha washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za ununuzi na kuratibiwa na  Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma Serikalini (PPRA).

"Umuhimu  wa mafunzo hayo ni kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa  kuondoa changamoto za wanunuzi  ambazo zilikuwa zikiwakabili  baada ya Serikali kufanya maboresho ili kuhakikisha upatikanaji wa thamani ya fedha ya manunuzi kwa umma ,"amesema.

Amesema Serikali ya awamu ya sita imeonyesha jitihada mbalimbali za  kutekeleza ujenzi wa mfumo wa manunuzi kwa umma kupitia mfumo wa Nest, ili kutimiza malengo yake katika kuhakikisha uwazi ,uwajibikaji na thamani ya fedha .

"Jitihada hizo ni pamoja na kuhakikisha ununuzi wa umma unazingatia uwazi,uwajibikaji, haki na kuongeza ufanisi kama sehemu ya kuleta mageuzi katika tasnia ya ununuzi nchini kwa kugeukia matumizi ya mfumo huo,"amesema Malisa.

Katika hatua nyingine  Malisa amesema  mafunzo hayo  yatakuwa chachu ya  watumishi kuziba ombwe la usimamizi mbovu wa mikataba katika Taasisi zao.

"Natarajia mtakwenda kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na  kuzingatia msingi mkuu wa kuwezesha upatikanaji wa Maendeleo ya Taifa na kulinda kwa wivu mkubwa rasilimali  zetu na teknolojia za kisasa,"amesema Rc Malisa.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,  Pascal  Manono  amesema lengo ni kuboresha mfumo wa manunuzi ili kuhakikisha kuna kuwepo na usimamizi mzuri wa mikataba ili kudhibiti malalamiko.

"Ni mafunzo endelevu ambayo yanafanywa kikanda ili kuhakikisha watumishi wote wa umma nchini wanayapata  licha ya kuwepo kwa   changamoto za baadhi kushindwa kushiriki kutokana na taasisi zao kushindwa kugharamia ,"amesema.

Ametaja malengo ni  kuzijengea uwezo taasisi nunuzi zote nchini kujua mfumo matumizi ya Nest, katika hatua za  kuanza kuchakata zabuni hadi kumamilisha mikataba .

"Pia kutakuwa na eneo la kufundishia suala la upekuzi wa mikataba ambalo litahusisha wanasheria na wazabuni kuona mikataba kwa maslai yao na taasisi husika,"amesema.


Kuhusu idadi ya walengwa

Manono amesema lengo ni kuwafikia watumishi wote wa umma waajiriwa na kuweka bayana kuwepo kwa ajenda ya majadiliano  sambamba na kushirikisha makundi maalumu.