Siku ya Ufaransa yaadhimishwa Dar, Serikali ikiainisha mafanikio iliyoyapata kupitia ushirikiano nayo
Dar es Salaam. Nchi ya ufaransa kupitia ubalozi wake nchini, imeadhimisha siku ya kimataifa ya nchi hiyo huku serikali ikieleza namna ilivyopata mafanikio tangu ilipoanzisha mashirikiano na nchi hiyo miaka ya 1961,utalii ,sekta ya maji vikitajwa .
Akizungumza katika sherehe za maadhimidho hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dennis Londo, amesema Tanzania inathamini mchango wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), ambalo limekuwa likifanya kazi nchini tangu mwaka 1993.
Londo amesema kuanzia mwaka 1993 hadi 2024, Ufaransa imechangia takribani euro bilioni 1.27, sawa na zaidi ya Shilingi trilioni tatu kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta za maji, nishati, uchukuzi, elimu na afya.
"Ushirikiano huu umeleta manufaa kwa uchumi wa Tanzania na Ufaransa kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali. Huu ndio ushirikiano wa kunufaishana ambao Tanzania inaendelea kuuhimiza,"amesema Waziri huyo.
Kuhusu sekta ya maji Waziri huyo amepongeza uzinduzi wa Mradi wa Kiwanda cha Kusafisha Maji cha Butimba uliofanyika Juni 2025 mradi ambao amesema unaofadhiliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania, Umoja wa Ulaya na Serikali ya Ufaransa ambao utaboresha upatikanaji wa maji safi na huduma za usafi kwa zaidi ya watu 450,000 wa Mwanza na maeneo jirani.
Kwenye sekta ya madini,Balozi Londo amesema
Katik kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la watalii kutoka Ufaransa ambapo M
Mwaka 2024 pekee zaidi ya watalii 150,000 walitembelea Tanzania Bara na Zanzibar.
"Tunatarajia idadi hiyo kuongezeka zaidi mwaka 2025, hasa kutokana na safari za moja kwa moja za ndege kati ya Ufaransa, Dar es Salaam na Zanzibar, pamoja na kufunguliwa tena kwa safari za moja kwa moja kuelekea Kilimanjaro mwezi Novemba 2024 baada ya kusimama kwa miaka 28,,"amesema.
Hata hivyo Londo ameongeza kuwa ingawa nchi zote mbili zimebarikiwa vivutio vya kipekee vya utalii, Ufaransa bado inaongoza duniani kwa kuvutia watalii wengi zaidi huku akiahidi Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya Ufaransa kupanua ushirikiano katika sekta hiyo.
Kuhusu diplomasia ya uchumi, tunafurahishwa kuona biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa ukiendelea kukua kila mwaka, huku fursa za kupanua ushirikiano huo zikiwa bado nyingi. Katika miaka ya karibuni, tumeshuhudia ujumbe wa wafanyabiashara kutoka pande zote mbili ukishiriki katika majukwaa ya biashara yaliyofanyika Tanzania na Ufaransa, jambo lililoimarisha zaidi mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi zetu.
Wakati kwenye sekta ya ulinzi, amesema anapenda kutambua ushirikiano huo katika sekta ya ulinzi na usalama, ambao umeendelea kuwa imara katika ngazi za pande mbili, kikanda na kimataifa.
Kwa upande wake balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Anne Sophie Ave, amesema sherehe hizo zimeendelea kuwa ishara ya umoja na misingi ya Jamhuri ya watu wa Tanzania na Ufaransa
Katika hotuba yake, amewataka raia wa ufaransa kutambua kwamba wao sio wafaransa kwa sababu tu wanaonekana Mfaransa, bali kwa sababu walizaliwa Ufaransa na u
wamechagua kuwa wafaransa."
Amesema hiyo ni kutokana na ukweli kuwa utambulisho wa Kifaransa haujengwi kwa muonekano, bali kwa uraia, huku akishauri k uwepo utambuzi wa Ufaransa kwa uraia wa nchi mbili au zaidi.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na watu mbalimbali ukiacha wanadiplomasia, pia walikuwepo viongozi wa biashara na watu mashuhuri kutoka katika tasnia ya sanaa.
ambapo mrembo Hamisa Mobetto, wasanii wa muziki Ommy Dimpoz na Ben Pol walikuwepo.
Pia kulikuwa na maonyesho ya kidijitali yaliyokuwa yakionyeshwa wakati wote yaliyoangazia kazi na miradi ya Ufaransa nchini Tanzania, ikiwemo Shindano la Ubunifu wa Khanga, Mpango wa Wasaidizi wa Lugha, Mkutano wa Africa Forward Summit, pamoja na ushirikiano katika sekta za afya, maji, nishati na nyinginezo.