Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakosoaji hatarini Pakistan

Imeelezwa kuwa watu wa kada mbalimbali wanaoikosoa serikali ya Pakistan wanajikuta katika wakati mgumu huku baadhi wakikamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Hayo yamebainishwa na mtetezi wa haki za binadamu nchini Pakistan, Razak Ibrahim katika mkutano wake na waandishi wa habari wakati akisoma azimio lao la pamoja ambalo serikali ya Pakistan ililijibu, ikibainisha kuwa maoni yao yanafanyiwa kazi.

‘’Tulikaa tukajadiliana na kutoka na tamko la pamoja kama watetezi wa haki za binadamu, tuliiandikia barua serikali kueleza kuwa kuna tatizo katika utatuzi wa masuala mbalimbali ya kijamii..., ukweli hauwekwi wazi na hata vyombo vya habari vinavyoripoti vinaminywa sana,’’

‘’Tulieleza kuwa hata waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan alikwenda jela kwa sababu ya kuikosoa serikali na mahakama. Sasa ukosoaji haupaswi kuwa kesi au uadui, sisi ni Wapakistan na tunazungumza kwa ajili ya taifa letu,’’ alisema Ibrahim.

Hivi karibuni mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa, Alice Jill Edwards alionya kuhusu watu kukamatwa wanapohoji masuala nyeti na kusisitiza kuwa mabadiliko ya 27 ya Katiba ya nchi hiyo yamechangia kuibua hali ya sintofahamu.

"Marekebisho ya 27 ya katiba ni shambulio baya dhidi ya uhuru wa mahakama na utawala wa sheria," alisema Edwards akinukuu maneno ya Tume ya Kimataifa ya Wanasheria (ICJ).

Katibu mkuu wa ICJ, Santiago Canton naye alizungumzia marekebisho ya katiba hiyo akisisitiza, ‘’yataathiri kwa kiasi kikubwa uwezo wa mahakama wa kuwawajibisha watendaji na kulinda haki za msingi za binadamu za watu wa Pakistani."

ICJ ilieleza baadhi ya kasoro ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Katiba ya Shirikisho (FCC), uteuzi wa jaji mkuu wa FCC, jaji mkuu wa mahakama kuu na mahakama ya katiba ya shirikisho, muundo wa tume ya mahakama ya Pakistan na uhamisho wa majaji wa mahakama kuu.