Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi wakumbushwa njia za kujinusuru na majanga

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni, Amani Hassan, akitoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu za kukabiliana na majanga ya dharura. Alikuwa amevaa kofia nyeusi wakati wa zoezi hilo.

Muktasari:

  • Wananchi wametakiwa kuwa na vifaa vya dharura majumbani, milango ya kutokea haraka na madirisha salama ili kujinusuru wakati wa majanga kama moto na mafuriko.

Dar es Salaam. Watanzania wamekumbushwa kuzingatia mbinu sahihi za kukabiliana na majanga ya dharura, ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa vinavyoweza kusaidia kuokoa maisha wanapokumbwa na hatari majumbani.

Miongoni mwa mbinu hizo ni kuwa na vifaa kama vitu vizito vinavyoweza kusaidia kubomoa ukuta au mlango ili kurahisisha njia ya kutokea wakati wa dharura. Pia, wananchi wametakiwa kuhakikisha nyumba zao zina milango ya dharura inayofunguka kwa nje pamoja na madirisha yanayoweza kutumika kujinusuru.

Akizungumza leo Aprili 25, 2026 jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni, Amani Hassan, amesema ni muhimu wananchi kuzingatia usalama tangu hatua ya ujenzi wa makazi yao.

“Ni muhimu kuhakikisha nyumba zinajengwa katika maeneo yanayofikika kwa urahisi na kuwa na njia za dharura. Wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu hatua za kujinusuru,” amesema.

Ameongeza kuwa uwepo wa vifaa vya kusaidia kuvunja kuta au milango unaweza kuwa msaada mkubwa wakati wa hatari.

Kwa wakazi wa maeneo yanayokumbwa na mafuriko, Kamanda Hassan amesisitiza umuhimu wa kuwa na vifaa kama kamba kwa ajili ya uokoaji wa haraka pamoja na kutunza mazingira ili kuzuia madhara ya mafuriko.

“Ni muhimu kuhakikisha njia za maji zinakuwa wazi wakati wote, kwani mafuriko hutokea maji yanapokosa njia ya kupita,” amesema.

Kwa upande wake, mwakilishi wa taasisi ya Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light (HWPL) nchini, Dk Erick Martin, amesema wanaendelea kutekeleza shughuli za kijamii zinazolenga kuimarisha mshikamano, upendo na amani.

Amesema kupitia idara ya vijana, taasisi hiyo imekuwa ikiandaa shughuli za usafi katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Standi ya Mwenge, kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika ili kuboresha mazingira na kuzuia magonjwa ya mlipuko.

Naye Kelvin Azoum, mmoja wa washiriki, amesema elimu waliyoipata imekuwa na manufaa makubwa, hasa katika uelewa wa ujenzi salama.

“Nyumba nyingi hujengwa bila kuzingatia tahadhari za dharura, jambo linaloweza kusababisha madhara makubwa pindi majanga kama moto yanapotokea,” amesema.