Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Washindi wa CRDB Bank Supa Cup wapitikana

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Group, Abdulmajid Nsekela (aliyesimama wa tatu kutoka kushoto) akia katika picha ya pamoja na timu ya Ulipo Tupo ambayo wameshinda ubingwa wa CRDB Supa Cup kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. Timu hiyo iliifunga CRDB Wakala kwa bao 1-0

Arusha. Katika kuendeleza juhudi za kuimarisha mshikamano kazini, kukuza afya njema na kuinua morali ya utendaji kazi miongoni mwa watumishi wake, Benki ya CRDB imehitimisha rasmi mashindano ya CRDB Bank SUPA Cup 2025 kwa fainali kubwa iliyofanyika katika Uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Fainali hiyo imewakutanisha watumishi wa benki hiyo kutoka kanda mbalimbali za Tanzania, wakishiriki katika michezo ya mpira wa miguu na netiboli, katika siku iliyojaa ushindani, burudani na mshikamano wa hali ya juu.

Hafla hiyo iliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Group, Abdulmajid Nsekela, na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa CPA (T) Amos Makalla.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Group, Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa michezo ni sehemu ya mkakati wa benki katika kujenga taasisi imara na yenye watu wenye afya na mshikamano.

“Michezo ni jambo la kimkakati kwa CRDB Bank. Imejikita ndani ya sera na utamaduni wetu wa kazi. Kupitia mashindano haya, tunajenga nidhamu, mshikamano na uongozi miongoni mwa watumishi wetu,” amesema Nsekela.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa CRDB Bank, Godfrey Rutasingwa, amesema kuwa benki inaendelea kuwekeza kwenye michezo kwa sababu inaelewa uhusiano mkubwa kati ya afya ya mwili na ubora wa utendaji kazi.

“Tunaamini michezo ni afya, na afya njema inazaa wafanyakazi wenye nguvu, umakini na tija. Hawa ndio wanaojenga taasisi imara na kutoa huduma bora kwa wateja,” amesema Rutasingwa.


Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Amos Makalla, ameipongeza CRDB Bank kwa kuonyesha mfano bora wa kuthamini watumishi wake na kuhimiza umoja nje ya mazingira ya kazi.

“CRDB Bank imeonyesha umuhimu wa kuwaleta watumishi pamoja nje ya majukumu ya kazi. Hii inawapa nafasi ya kupumzika, kuimarisha mahusiano na kurejea kazini wakiwa na nguvu mpya na ari ya kufanya kazi kwa ubora zaidi,” amesema Makalla.

Mashindano ya mwaka huu yalihitimishwa kwa michezo mikali ya fainali, ambapo Ulipo Tupo FC (Lake Zone) walitwaa ubingwa wa mpira wa miguu, huku Popote Inatiki Queens (Central Zone) wakitwaa ubingwa wa netiboli. Mafanikio hayo yaliambatana na zawadi nono pamoja na kutambua wachezaji binafsi waliofanya vizuri zaidi.

Kadri jua lilivyotua jijini Arusha na vigelegele vikapungua, jambo moja lilibaki wazi, CRDB Bank SUPA Cup 2025 haikuwa tu mashindano ya michezo, bali jukwaa la kuunganisha watu, kujenga afya, na kuimarisha utamaduni wa kazi wa pamoja.

Mwisho wa mashindano haya ni mwanzo wa safari mpya, huku macho yote yakielekezwa kwenye CRDB Bank SUPA Cup 2026.