Wateja watatu CRDB kushuhudia mechi za Kombe la Dunia Canada
Dar es Salaam. Jumla ya wateja watatu wa Benki ya CRDB wamejishindia tiketi za kushuhudia moja kwa moja mechi ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Canada kupitia kampeni ya Fainali Ndo Mpango na TemboCard Visa.
Washindi hao ni Godfrey Chibulunje, Habiba Sarah Filikunjombe na Lenah Munyua ambao wote wanatoka Mkoa wa Dar es Salaam.
Washindi hao wanaungana na wengine watatu ambao walishinda droo ya pili na kufanya jumla kuwa sita ambao wataona mechi 'live' nchini Canada.
Washindi wengine wanne wataona mechi 'live' nchini Marekani hivyo kufanya jumla ya washindi 10 kuhudhuria mechi hizo kupitia kampeni ya benki ya CRDB.
Mbali na zawadi hiyo kubwa, wateja wengine wanne ambao ni Kayn Senga wa Dar es Salaam, Faik Said Khamis Zanzibar) na Athumani Ali Omari wa Dar es Salaam wamejishindia televisheni ya Hisense ya inchi 85 king’amuzi na kifurushi kitakachowawezesha kufuatilia mechi zote za fainali za Kombe