Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amekanusha madai ya Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk Hamisi Kigwangalla kuwa mabehewa ya treni ya kisasa yaliyoletwa nchini ni mtumba.


Novemba 25 TRC ilipokea mabehewa 14 kati ya 59 ya masafa marefu, huku pia ikitarajia kupata vichwa 10 vya treni ya umeme (EMU).


Akizungumza jana jijini Dodoma baada ya kufanya safari ya majaribio ya treni kutoka Dar es Salaam wakiwa na wenyeviti wa CCM, Kadogosa amesema, mabehewa yaliyoletwa si mtumba na yule anayedai hivyo aulizwe vyanzo vya taarifa hizo.