Baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa Chadema wamesisitiza chama hicho kuanza mikutano ya hadhara, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.


Desemba 15 mwaka huu, akizungumza katika mkutano wa uchaguzi wa Bunge la wananchi la Chadema uliofanyika Dar es Salaam, Mbowe alisema chama hicho kinaendelea na maridhiano na CCM, huku akiwataka viongozi wenzake kuendelea na mikakati ya kisiasa ya kujiimarisha.