Mwenyekiti wa Kampuni ya National Media Group (NMG), Dk Wilfred Kiboro amesema zaidi ya nchi 17 za Afrika zimekubali na kuunga mkono mpango wa kuwa na ‘Soko la Usafiri wa Anga la Afrika (SAATM)’.

Hayo ameyasema leo Alhamis Desemba 8, 2022 wakati akizungumza kwenye tamasha la ‘Kusi Ideas Festival’ lililoandaliwa na NMG linalofanyika Nairobi nchini Kenya.