Rais Samia Suluhu Hassan ameingilia kati sakata la mabehewa lililoibua gumzo kwenye mitandao ya jamii na vyombo vya habari, akisema hata kama mabehewa yalishatumika, basi yamekarabatiwa vizuri kutoa huduma.

Hivi karibuni, Serikali imenunua mabehewa 39 ambapo kati yake 14 ni ya reli ya kisasa (SGR) na mengine 22 ni ya reli ya kawaida.