Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi) Innocent Bashungwa ameagiza kusimamishwa kazi na kuhojiwa na Taasisi Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) watumishi watano kutokana kuisababishia hasara Halmashauri ya Wilaya Kiteto Mkoani Manyara.