Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi hapa sababu ZRA kuvuka lengo makusanyo ya mwaka kwa asilimia 101

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Said Athumani Kiondo akitoa taarifa ya makusanyo ya mwaka wa fedha 2024/25 makao makuu ya Mamlaka hiyo Unguja

Muktasari:

  • Kwa mwaka wa fedha 2024/25 ilikadiriwa kukusanya Sh845 bilioni ila imekusanya Sh861 bilioni sababu kubwa ikitajwa ni kuongeza kwa shughuli za kiuchumi visiwani humo.

Unguja. Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), imefanikiwa kukusanya Sh861.882 bilioni katika mwaka wa fedha 2024/25, ikiwa ni zaidi ya lengo la Sh845.979 bilioni.

Hii ni sawa na ufanisi wa asilimia 101.88 ya lengo la makusanyo yaliyopangwa.

Kamishna Mkuu wa ZRA, Said Athumani Kiondo ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumanne Julai 1, 2025.

Kiondo amesema mafanikio hayo yametokana na uboreshaji wa mifumo na mikakati ya kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari.

Amesema makusanyo hayo yameongezeka kwa asilimia 19.91, sawa na Sh143.122 bilioni, ikilinganishwa na makusanyo halisi ya mwaka wa fedha 2023/24 ambayo yalikuwa Sh718.760 bilioni.

Kuhusu makusanyo ya robo ya nne ya mwaka wa fedha 2024/25, Kiondo amesema ZRA ilikadiria kukusanya Sh188.164 bilioni lakini imekusanya Sh194.103 bilioni, ufanisi wa asilimia 103.16 ya lengo.

Amesema ukilinganisha na robo ya nne ya mwaka wa fedha uliopita 2023/24 ambayo ilikusanya Sh159.276 bilioni, kuna ongezeko la Sh34.827 bilioni sawa na ukuaji wa asilimia 21.87.

“Kwa Juni 2025 pekee, ZRA ilikuwa imetabiri kukusanya Sh56.646 bilioni lakini imekusanya Sh63.670 bilioni, sawa na ufanisi wa asilimia 112.40. Aidha, makusanyo ya Juni 2025 yakilinganishwa na Juni 2024 (Sh48.896 bilioni) yanaonyesha ongezeko la Sh14.775 bilioni, sawa na ukuaji wa asilimia 30.22,” amesema.

Sababu za mafanikio
Akieleza kuhusu vyanzo vya mafanikio hayo, Kiondo amesema yamechangiwa na kuimarika kwa shughuli za kiuchumi kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, kunakotokana na sera na uongozi mzuri wa viongozi wakuu wa kitaifa.

“Uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa miundombinu na huduma za kijamii, pamoja na kuimarika kwa shughuli za kiuchumi Zanzibar kutokana na utekelezaji wa sera bora za kiuchumi, umechangia kwa kiasi kikubwa,” amesema Kiondo.

Aidha, ametaja kuimarika kwa mikakati ya ukusanyaji kodi, ikiwemo matumizi ya teknolojia na programu za kisasa kama moja ya sababu za kuongeza ufanisi wa makusanyo.

Mikakati kwa mwaka 2025/26
Akizungumzia mipango ya mwaka wa fedha 2025/26, amesema ZRA imepangiwa kukusanya jumla ya Sh1.257 trilioni.

Ili kufikia lengo hilo, amesema ZRA itatekeleza mikakati kadhaa, ikiwemo kutoa msamaha wa adhabu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni yatokanayo na kuchelewa au kutolipa kodi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya alipowasilisha Bajeti Kuu ya Serikali Juni 12, 2025, alieleza kuwa misamaha hiyo ya adhabu za kodi itatolewa kwa asilimia 100 kuanzia Julai 1 hadi Desemba 31 mwaka huu.

“Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa Sh12.57 bilioni,” alisema Dk Saada.

Kiondo aliongeza kuwa ZRA itaendeleza kampeni za kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kwa njia tofauti ili kuongeza uelewa na utii wa ulipaji kodi.