Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi amuapisha Mansura kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

Mansura Mossi Kassim akila kiapo cha kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Muktasari:

  • Mansura anakua mwanamke wa pili kushika wadhifa huo Zanzibr akitanguliwa na Zena Said aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo tangu Rais Mwinyi aingie madarakani awamu ya kwanza mpaka Machi mwaka huu alipoteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amemuapisha Mansura Mossi Kassim kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Hafla hiyo imefanyika leo Jumatano, Juni 24, 2026 Ikulu Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Kabla ya uteuzi huo, Mansura alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora.

Mansura anachukua nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said ambaye aliteuliwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia.

Zena aliteuliwa kushika nafasi ya ukatibu mkuu kiongozi mwaka 2021 baada ya Rais wa Zanzibar, Dk Mwinyi kuingia madarakani hadi Machi, mwaka huu, alipoteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nafasi ya ubalozi huko Saudi Arabia.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi wakati akimuapisha Mansura Mossi Kassim kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). leo Jumatano, Juni 24, 2026 Ikulu Zanzibar


Mjue Mansura

Katika utumishi wake Mansura amabaye ameamza kutumikia nafasi hiyo leo, alikuwa mfanyakazi wa kawaida katika wizara ya Killimo na Mifugo na kujiendeleza kimasomo akiwa kazini baadaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wizara katika wizara hiyo wakati wa utawala wa Rais wa Awamu ya saba, Dk Ali Mohamed Shein.

Baada ya Rais Mwinyi kuingia madarakani, mwaka 2020, alimteua kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora mpaka mwaka jana alipomteua kuwa katibu mkuu kamili wa Wizara hiyo nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Seif Shaaban ambaye alihamishiwa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Umwagiliaji hadi alipostaafu.