Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkakati wawekwa kuvutia diaspora kuwekeza Zanzibar

Mkurugenzi wa wateja binafsi, wafanyabiashara wadogo na wakati kutoka Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Lilian Mtali (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa CPS Afrika Fumba Town, Sebastian Dietzold wakisaini makubaliano ya kurahisisha  Diaspora katika kushiriki katika kukuza uchumi wa Zanzibar katika Jukwaa la Uwekezaji Zanzibar Unguja

Muktasari:

  • Hii ni baada ya Serikali kuweka mazingira mazuri kwao huku yakiingiwa makubaliano maalumu ya kurahisha upatikanaji wa nyumba za uwekezaji katika mji wa kisasa Fumba Town.

Unguja. Wakati Serikali ikieleza dhamira yake kuendelea kuweka mazingira bora kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) kushiriki katika uwekezaji, Benki ya Biashara (TCB) imesaini makubalino na Kampuni ya CPS Afrika kurahisisha ushiriki wao katika maendeleo ya uchumi wa nchi.

Akizungumza leo Juni 5, 2026 wakati wa mjadala wa diaspora katika jukwaa la uwekezaji Zanzibar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Dk Saada Mkuya Salum, amesema Serikali imefungua fursa ya ushirikishwaji wa wanadiaspora katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji, biashara, utalii pamoja na kukiimarisha Kiswahili.

 “Serikali inaendelea kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyowakabili diaspora ili kuwapa nafasi pana zaidi ya kuwekeza katika sekta tofauti za uchumi hapa Zanzibar,” amesema.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya benki hiyo na CPS Fumba Town, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki amesema makubaliano hayo yanafungua njia kwa wana diaspora kupata mikopo au uwezeshaji wa kununua nyumba 

“Mradi huo upo kwenye eneo la ‘economic zone’ hata diaspora ambao ni raia wa nchi nyingine wanaweza kununua katika eneo hilo na kufanya uwekezaji,” amesema. 

“Nitoe rai kwa wanadiaspora wenye nia ya kumiliki nyumba hapa Zanzibar ama kwa matumizi binafsi au kwa matumizi ya uwekezaji kwa sababu mahitaji ni makubwa maana malengo ya Serikali ni kuongeza watalii, kwa hiyo kutakuwa na mahitaji makubwa ya malazi,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa wateja binafsi, wafanyabiashara wadogo na wakati kutoka TCB, Lilian Mtali, amesema ushirikiano huo wa kimkakati umelenga kurahisisha upatikanaji wa nyumba na fursa za uwekezaji wa mali isiyohamishika.

 Pia, amesema ni hatua ya kimkakati inayounganisha huduma za kifedha na sekta ya maendeleo ya makazi, kuwawezesha diaspora na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kupata fursa za umiliki wa nyumba katika mazingira salama, ya kisasa na yenye thamani ya muda mrefu.

Amesema kupitia ushirikiano huo mpya, wateja wa diaspora pamoja na wawekezaji wa kimataifa watapata fursa ya kuwekeza katika miradi ya makazi ya kisasa ya Fumba Town, ambayo imekuwa ikivutia wawekezaji wengi kutokana na miundombinu yake bora na mazingira yake yanayokua kwa kasi.

Naye Mtendaji Mkuu wa CPS Africa, Fumba Town Sebastian Dietzold amesema Fumba Town ni mji wa kisasa ambao unakuwa kwa haraka hapa Zanzibar na ina nyumba nyingi kwa ajili ya uwekezaji, watu kuishi na kufanya biashara.

Amesema ni faraja kusaini mkataba huo kati yao na TCB ili kupata mkopo na kununua nyumba hapa Zanzibar hiyo itasaidia diaspora kupata njia rahisi ya uwekezaji nyumbani kwao.

“Sisi tunatengeneza nyumba nyingi na tayari tumeshamaliza nyumba zaidi ya 1,000 na Fumba Town wapo watu zaidi ya 3,000 wanaishi hapa Zanzibar na wawekezaji zaidi ya nchi 70 duniani wamekuja kuwekeza hapa,” alisema.

Hivyo, amewasihi wanadiaspora kuchangamkia fursa hiyo kwani Zanzibar ina fursa nyingi za uwekezaji ni salama.