Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mwinyi ataja sababu za kuwekeza Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, akifungua Jukwaa la Wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani kujadili fursa za uwekezaji na maendeleo ya uchumi, Unguja, Zanzibar.

Muktasari:

  • Miongoni mwa sababu hizo ni uwepo wa uthabiti wa sera, nafasi ya kimkakati, nguvu kazi na vijana wenye nguvu, faida za asili na za ushindani na Serikali kuwa mshirika badala ya kuwa mdhibiti tu

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametaja mambo matano visiwani humo kuwa sehemu sahihi ya kuwekeza hasa kuboresha miundombinu.

Miongoni mwa mambo hayo ni uthabiti wa sera, nafasi ya kimkakati, nguvu kazi na vijana wenye nguvu, faida za asili na za ushindani na Serikali kuwa mshirika badala ya kuwa mdhibiti tu.

Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Juni 4, 2026 wakati akifungua jukwaa la uwekezaji Zanzibar ambalo limewakutanisha washiriki 700 kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwamo watunga sera, wawekezaji, wafanyabaishara, sekta binafsi na washirika wa amendeleo.

“Tumeweka mageuzi ambayo yanalinda wawekezaji, kurahisisha taratibu na kuhakikisha uthabiti katika utekelezaji wa sera. Uwekezaji wako uko salama hapa,” amesema.

“Zanzibar ipo makutano ya Afrika, Asia na Mashariki ya Kati, uwanja wa ndege  Uwanja wetu wa ndege ulioboreshwa na miradi ya bandari ya maji marefu vinaiweka kama kituo cha vifaa na biashara kwa kanda na zaidi.

“Kwa upande wa nguvu kazi, zaidi ya asilimia ya watu wetu wana umri chini ya miaka 35. Tunawekeza katika mafunzo ya ufundi, ujuzi wa kidijitali, na ujasiriamali kuhakikisha watu wetu wako tayari kuendesha viwanda vipya,” amesema.

Amesema Serikali imekuwa mshiriki badala ya kuwa mdhibiti tu, hivyo kupitia Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (Zipa) na taasisi nyingine, wanatoa huduma ya kituo kimoja, huduma za baada ya uwekezaji na mawasiliano ya moja kwa moja na wawekezaji.

Akizungumzia mada ya mkutano huo isemayo “Kukuza Uwekezaji, Utofautishaji, Maendeleo Endelevu Zanzibar: Kuunda Hadithi Mpya ya Ukuaji wa Zanzibar, Dk Mwinyi amesema inaakisi mwelekeo wa sera uliopangwa kwa makusudi.

 “Si kauli mbiu ya kibiashara. Inabeba uamuzi wa kimkakati ambao Serikali hii imeufanya; kupanua msingi wa uchumi wetu, kupunguza utegemezi wa sekta moja na kujenga msingi wa kiuchumi unaostahimili mabadiliko kwa wenye tija zaidi na wenye manufaa kwa watu wetu,” amesema.

Amesema wamewekeza kwa kiasi kikubwa katika barabara, viwanja vya ndege, bandari, uzalishaji wa umeme, huduma za utalii na huduma za umma.

Waziri wa Ajira na Uwekezaji, Shariff Ali Shariff amesema kupitia jukwaa hilo wanatafuta kujenga ushirikiano wa kudumu utakaoharakisha maendeleo ya viwanda, upanuzi wa miundombinu, ukuaji wa utalii, mabadiliko ya kidijitali, uwekezaji na nishati mbadala.

Mkurugenzi wa Zipa, Saleh Saad Mohamed amesema wanaendelea kujitolea kuwawezesha wawekezaji kupitia huduma bora msaada wa sera na uratibu.

“Tunaamini uwekezaji si suala mtiririko wa mtaji tu, ni kujenga ushirikiano endelevu unaounda fursa kwa kuhamisha maarifa kuiwezesha jamii na kuchangia ustawi wa Taifa,” amesema.

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC), Ali Amour amesema tangu Rais Mwinyi aingie madarakani ameonesha ukuaji endelevu unatokana na ushirikiano thabiti kati Serikali na sekta binafsi.

Amesema imani yake katika uchumi unaoendeshwa na sekta binafsi imeimarisha imani ya wawekezaji na kuiweka Zanzibar kuwa kituo kinachovutia zaidi kwa wawekezaji wa ndani na nje.

Amesema fursa ni kubwa ingawa utalii bado ni uti wa mgongo, mustakabali upo katika uchumi wa buluu usindikaji mazao, uvuvi, viwanda, nishati mbadala vifaa vya uchukuzi, ufumbuzi, wa kidijitali, hudUma za kifedhana uchumi wa maarifa.

“Tunakaribisha kwa dhati sheria ya maendeleo ya sekta binafsi, itatupa mfumo kisheria na kitaasisi tunaohitaji. Sheria hiyo ikishapita, sekta binafsi ipo tayari kuwekeza zaidi, kubuni zaidi, kuunda ajira na kuharakisha dira ya Zanzibar 2050,” amesema Amour.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Dorota Panczyk amesema umoja huo ni mshirika wa muda mrefu na wa kuaminika wa Tanzania na Zanzibar ambapo ushirika wao unaangazia vipaumbele walivyonavyo kwa pamoja, ikiwa ni ukuaji endelevu na jumuishi, utofautishaji wa uchumi, kuongeza thamani ya ndani na uundaji wa ajira hasa kwa vijana.

"Ushirikiano wetu umejengwa juu ya kanuni za pamoja, maadili ya kidemokrasia utawala bora na uwazi. Hizi ni muhimu kwa mazingira ya biashara yenye utabiri, utulivu na uendelevu ambayo ndio ufunguo wa kuvutia uwekezaji binafsi,” amesema.